Loading...
title : UPASUAJI WAANZA KUFANYIKA HOSPITALI ZA VIJIJINI MANONGA
link : UPASUAJI WAANZA KUFANYIKA HOSPITALI ZA VIJIJINI MANONGA
UPASUAJI WAANZA KUFANYIKA HOSPITALI ZA VIJIJINI MANONGA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali ameeleza hali ya afya katika jimbo la Manonga na hii ni baada ya mikakati ya kuboresha huduma za afya katika vijiji vyote Jimboni humo.
Akifanya mahojiano na blogu ya jamii Gulamali amesema kuwa: "Ni furaha yetu kuona Upasuaji unafanyika katika vijiji vyetu na tuna washukuru Afrikan Dev Bank kwa kufanikisha hili. Kituo cha afya cha Choma Chankola tayari kimeshafanya upasuaji 69 na kati ya 69 ni 1 tu ndio iliyofeli na hiyo ni kutokana na mzazi kuchelewa kufika Kituoni hali iliyopelekea Upasuaji wake kufanikisha mtoto mmoja na mama kuwa hai na mtoto mwingine kupoteza maisha, lakini zilizobaki zote 68 zilienda Vizuri" ameeleza Gulamali.
Kuhusiana na huduma za upasuaji zinazopatikana katika Kituo hicho cha Afya Gulamali amesema ; "Upasuaji wa kutoa mawe tumboni, kujifungua, na upasuaji kwa watoto na huduma zote hizo zinafanyika katika kituo chetu cha afya Choma" ameeleza.
Aidha ameeleza kuwa hayo ni maendeleo makubwa sana, kilichobaki ni kuongeza majengo hasa ya mama na mtoto, jengo la kuhifadhia maiti, maabara, jengo la Ufuaji na Nyumba za Watumishi na hiyo ni Sambamba na kuongeza madaktari na wauguzi.Hata hivyo anamshukuru Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa ziara yake kwa kutoa Fedha za Kuboresha Kituo hicho cha Afya cha Choma Chankola.
Pia amesema kuwa; "Ni matumaini yetu Tutaweza pata hela kwa ajili ya hayo majengo, na nitumie nafasi hii kumpongeza Daktari Frank na wauguzi wote kituoni hapa kwa huduma zao wanazotoa" ameeleza.
Baadhi ya wananchi wamempongeza Mbunge huyo na kueleza kuwa amekuwa lulu kwa wana Manonga hasa kwa kutoa vipaumbele muhimu kwa Wananchi bila kujali itikadi zao na wamemtaka kuendelea na moyo na imani hiyo ya kuipeleka Manonga mbele zaidi.

Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akikagua baadhi ya majengo katika hospitali ya Choma Chonkola katika jimbo la Manonga.
Muonekano wa chumba cha upasuaji katika hospitali iliyopo katika kijiji cha Choma Chonkola.
Hivyo makala UPASUAJI WAANZA KUFANYIKA HOSPITALI ZA VIJIJINI MANONGA
yaani makala yote UPASUAJI WAANZA KUFANYIKA HOSPITALI ZA VIJIJINI MANONGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UPASUAJI WAANZA KUFANYIKA HOSPITALI ZA VIJIJINI MANONGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/upasuaji-waanza-kufanyika-hospitali-za.html
0 Response to "UPASUAJI WAANZA KUFANYIKA HOSPITALI ZA VIJIJINI MANONGA"
Post a Comment