Loading...

WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI

Loading...
WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI
link : WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI

soma pia


WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO 

Wadau wa Elimu wametakiwa kuendelea kufanya tathmini ya elimu kwa kujadili mafanikio na changamoto za sekta hiyo ili kuboresha na kukuza elimu nchini.

Hayo yamebainishwa jana jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Selemani Jafo alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Elimu.

Waziri Jafo amesema kuwa nchi nyingi ambazo hazina rasilimali za madini wala vivutio vya utalii zinaendelea kuwekeza katika rasilimali elimu ambapo baadae nchi hizo huwa tajiri na kutoa misaada kwa nchi masikini.

“Taifa linalowekeza vizuri katika sekta ya elimu ndilo Taifa lenye nafasi kubwa ya kukomboa wananchi wake na taifa kiujumla hivyo kutathmini juu ya elimu inayotolewa nchini kwetu ni jambo la muhimu sana”, alisema Jafo.

Waziri Jafo amewasisitiza wadau wa elimu walioshiriki katika mafunzo hayo kutekeleza maazimio yote yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ili kuendelea kutoa matokeo chanya katika sekta hiyo.

Vile vile ametoa rai kwa wadau wa elimu kuendelea kutoa michango yao ya hali na mali katika kuinyanyua sekta ya elimu nchini ili kwa pamoja taifa la Tanzania liweze kujinasua katika umasikini kupitia elimu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), Selemani Jafo akifunga Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akitoa neno la Utangulizi wakati wa ufungaji wa Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu. 
Baadhi ya wadau wa elimu walioshiriki katika Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.

Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi  walioshiriki kama Wadau wa Elimu katika Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu. 
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Lydia Wilberd akitoa salamu za asasi hiyo kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.




Hivyo makala WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI

yaani makala yote WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/wadau-watakiwa-kuendelea-kufanya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI"

Post a Comment

Loading...