Loading...

WATAALAMU WA AFYA WAPEWA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO TeleECHO.

Loading...
WATAALAMU WA AFYA WAPEWA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO TeleECHO. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATAALAMU WA AFYA WAPEWA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO TeleECHO., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATAALAMU WA AFYA WAPEWA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO TeleECHO.
link : WATAALAMU WA AFYA WAPEWA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO TeleECHO.

soma pia


WATAALAMU WA AFYA WAPEWA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO TeleECHO.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Wizara ya Afya Maendelea ya Jamii  Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo CDC na Chuo Kikuu cha Mexico inaendelea kutoka mafunzo kwa njia ya mtandao kwa kutumia mfumo wa (TeleECHO) kwa wataalamu wa afya  ili kuwajengea uwezo pamoja na kupunguza gharama.

Akizungumza leo jiini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa njia ya mtandao, Mkurugenzi Uhakiki wa Huduma Bora za Afya Dkt Mohammed Ali Mohammed, amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia sana kuwafikia wataalamu wengi kwa muda mfupi.

Dkt Mohamed amesema mfumo kwa njia ya mtandao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya hasa maeneo ya vijijini.

Amesema mfumo huo utaweza kuwafikia watoa huduma kwa asilimia kubwa sambamba na kupunguza gharama za mikutano.

"Rais Dkt. John Magufuli alipozindua mtandao wa TTCL alisisitiza tuanze kutumia mafunzo kwa kupitia masafa ili kupunguza gharama za safari na kuhakikisha tunawafikia watu wengi kwa wakati mmoja ” amesema Dkt Mohamed.

 Dkt Mohamed ambaye alikuwa anamwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali amesema kuwa wizara kwa kushirikiana na wadau ina mikakati ya kufunga vifaa maalumu vya mfumo huo katika vituo vya afya vilivyopo katika hospitali za rufaa za mikoa ikiwemo Dodoma, Kagera, Pwani, Arusha, Tanga ambavyo  vitaunganishwa katika Hospitali  ya Taifa Muhimbili.

Dkt. Mohamed amefafanua kuwa  kwa mujibu wa sheria ya maabara namba 22 ya mwaka 2007 inawataka watu wote wanaofanya vipimo vya maabara wapatiwe leseni (certification).

Mkurugenzi wa Mafunzo Dkt. Donard Mbando amesema vituo vya afya vilivyoanza kutekeleza mpango huo wa kupata mafunzo hayo  ni pamoja na mkoa wa Shinyanga, Iringa, Njombe na Mbeya.

Dkt. Mbando ameishukuru wizara ya afya kwa mchango wao katika kufanikisha utekelezaji wa utoaji wa mafunzo kwa njia ya mtandao.

Mafunzo kwa njia ya mtandao yamewashirikisha wadau mbalimbali  Wizara ya Afya Maabara ya Taifa kutoka mikoani Dodoma, Morogoro pamoja na Hospitali ya Kibong’oto ya kifua kikuu.

Lengo la mafunzo hayo ni uhakikisha wataalamu wa maabara wanafanya kazi yao kwa uweledi hasa katika kuwapa majibu sahihi watu wanapopima virusi vya ukimwi.

Mfumo wa utoaji mafunzo kwa njia ya mtandao TeleECHO ulianza mwaka 2016 kwa kuanza kutumia katika hospitali nne za mikoa ambazo ni  Mbeya, Iringa, Njombe pamoja na Shinyanga.



Hivyo makala WATAALAMU WA AFYA WAPEWA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO TeleECHO.

yaani makala yote WATAALAMU WA AFYA WAPEWA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO TeleECHO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATAALAMU WA AFYA WAPEWA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO TeleECHO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/wataalamu-wa-afya-wapewa-mafunzo-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WATAALAMU WA AFYA WAPEWA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO TeleECHO."

Post a Comment

Loading...