Loading...

WAWILI WAFA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO MBALA HUKO CHALINZE

Loading...
WAWILI WAFA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO MBALA HUKO CHALINZE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAWILI WAFA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO MBALA HUKO CHALINZE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAWILI WAFA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO MBALA HUKO CHALINZE
link : WAWILI WAFA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO MBALA HUKO CHALINZE

soma pia


WAWILI WAFA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO MBALA HUKO CHALINZE


Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani (ACP)Wankyo Nyigesa ,akionyesha moja ya gari iliyoharibika vibaya,katika ajali iliyohusisha magari mawili ambayo yamegongana uso kwa uso , barabara ya Dar es salaam -Morogoro eneo la Mbala ,Chalinze Mkoani Pwani ,na kusababisha vifo vya watu wawili.(picha na Mwamvua Mwinyi)
4,septemba

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
WATU wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa ,katika ajali iliyohusisha magari mawili ambayo yamegongana uso kwa uso huko barabara ya Dar es salaam -Morogoro eneo la Mbala ,Chalinze Mkoani Pwani .
Akielezea kuhusiana na ajali hiyo ,kamanda wa polisi mkoani humo ,(ACP) Wankyo Nyigesa alisema, imetokea usiku wa kuamkia septemba 4 majira ya saa 9.30 alfajiri.
Alisema gari namba T.542 DMJ/ 680 DKS aina ya Howo mali ya kampuni ya Gulf Agent ikitoka Dar es salaam kuelekea Chalinze ikiendeshwa na dereva Ramadhani Kibingo ( 38) mkazi wa Mbagala iligongana na gari T.405 DLV/ 904 DMN aina ya Daf mali ya kampuni ya RAS Logistic (T) ltd iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Dsm ikiendeshwa na dereva bado kufahamika jina lake (35-40).
“Ajali hii imesababisha vifo vya dereva huyo aliyekuwa akiendesha gari yenye namba T.405 DLV/904 DMN aina ya Daf na tingo wake ambao bado nae kufahamika jina, mme ( 25 – 30 )” alisema Wankyo.
Wankyo aliwataja majeruhi kuwa ni dereva  Ramadhani Kibingo na tingo wake Ibrahim Said, Mzigua (28), mkazi wa Dar es salaam waliokuwa ndani ya gari T.542DMJ/680 DKS. 
Kwa mujibu wa kamanda huyo ,magari yote yameharibika kutokana na ajali hiyo iliyotokea.
Alisema ,miili ya marehemu imepelekwa hospital ya rufaa Tumbi kwa uchunguzi na kuhifadhiwa na majeruhi wamepelekwa kituoa cha afya Chalinze kwa ajili ya matibabu na hali zao sio mbaya. 
Dereva wa gari T.542 DMS/680 DKS aina ya Howo ,anashikiliwa chini ya ulinzi wa polisi kituo cha afya Chalinze. 
Chanzo cha ajali ni dereva huyo ambae anadaiwa alijaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhali na kugongana uso kwa uso na gari T.504 DLV/904 DMN aina ya Daf.
Wakati huo huo ,Wankyo alikemea ,madereva ambao sio makini na wanaoendesha bila tahadhali na kusema sheria itachukua mkondo wake kwa Dereva anaekiuka sheria za usalama barabarani .


Hivyo makala WAWILI WAFA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO MBALA HUKO CHALINZE

yaani makala yote WAWILI WAFA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO MBALA HUKO CHALINZE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAWILI WAFA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO MBALA HUKO CHALINZE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/wawili-wafa-na-wengine-kujeruhiwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAWILI WAFA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO MBALA HUKO CHALINZE"

Post a Comment

Loading...