Loading...

WEZI WA FEDHA ZA SERIKALI NYANG'WALE WATIWA MBARONI

Loading...
WEZI WA FEDHA ZA SERIKALI NYANG'WALE WATIWA MBARONI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WEZI WA FEDHA ZA SERIKALI NYANG'WALE WATIWA MBARONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WEZI WA FEDHA ZA SERIKALI NYANG'WALE WATIWA MBARONI
link : WEZI WA FEDHA ZA SERIKALI NYANG'WALE WATIWA MBARONI

soma pia


WEZI WA FEDHA ZA SERIKALI NYANG'WALE WATIWA MBARONI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiongea na Viongozi na wananchi wa Nyang'wale.
Madiwani wa Nyang'wale wakisikiliza maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea Halmashauri hiyo.

Watumishi sita pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Geita baada kubainika kuchezea fedha za miradi ya maendeleo zilizoelekezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale. 

Watu hao ni Aliyekuwa mkurugenzi wa Nyang'wale Calous, wahasibu Robert na Godson, Mweka Hazina Ronatus, Afisa habari Zahoro, Katibu wa Afya Alfred Joseph, na Afisa utumishi Muhando B.Mhando.

Wizi uliofanyika katika fedha za miradi ya Afya, Elimu, Jengo la Utawala, na Maji ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuna ubadhirifu wa Sh.Bilioni 2.2. 

Kushikiliwa kwa watumishi hao kumetokana na agizo alilolitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ambapo ameelekeza vyombo vya dola kufanya kazi yake na tayari wanashikiliwa na jeshi hilo. 

Jafo akiwa katika mkutano wa kikazi wilayani humo amevitaka vyombo vya Dola kusimamia vyema jambo hilo ili waliohusika mali zao zishikiliwe ili kufidia fedha zilizopotea sambamba na hatua zingine za kisheria. 

Hata hivyo Waziri Jafo amemtaka mwenyekiti wa Halmashauri hiyo pamoja na Makamu wake kujitafakari kama wanafaa kusimamia fedha za wananchi wa Nyang'wale. 

Aidha Waziri Jafo amepongeza Mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo Mariam Chaurembo kwa kubaini kwa haraka ubadhirifu huo wakati wa makabidhiano na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wa awali. 

Amewataka wakurugenzi nchini kuwa makini katika kusimamia majukumu yao.


Hivyo makala WEZI WA FEDHA ZA SERIKALI NYANG'WALE WATIWA MBARONI

yaani makala yote WEZI WA FEDHA ZA SERIKALI NYANG'WALE WATIWA MBARONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WEZI WA FEDHA ZA SERIKALI NYANG'WALE WATIWA MBARONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/wezi-wa-fedha-za-serikali-nyangwale.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WEZI WA FEDHA ZA SERIKALI NYANG'WALE WATIWA MBARONI"

Post a Comment

Loading...