Loading...
title : ALIYEKUWA RAIS WA MIGODI YA MADINI AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO
link : ALIYEKUWA RAIS WA MIGODI YA MADINI AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO
ALIYEKUWA RAIS WA MIGODI YA MADINI AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO
Na Karama Kenyunko, glogu ya jamii
ALIYEKUWA Rais wa Migodi ya Pangea, North Mara, exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika na Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo leo Oktoba 17.2018 wemefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya USD milioni 112.
Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao leo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kevin Mhina na Jopo la mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na Wakili wa serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro na Jackilline Nyantori.
Mbali na Mwanyika na Lugendo, washtakiwa wengine ni kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama 3, mashtaka yavkughushi 7.
Utakatishaji wa fedha 17, Kuwasilisha nyaraka za uongo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzanian (TRA), shtaka moja, kuongoza uhalifu wa kupangwa shtaka moja, kukwepa kodi, mashtaka 8 na shtaka moja la kutoa Rushwa.
Akisoma hati ya mashtaka wakili Nchimbi amedai washtakiwa hao pamoja na watu wengine ambao bado hawajakamatwa, walitenda makosa hayo kati ya Aprili 11.2008 na June 30.2007 katika sehemu tofauti za jiji la dar es Salaam, Kahama Mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini Uingereza.
Imedaiwa katika kipindi hicho na mahali huko washtakiwa hao kwa pamoja wakiwa na watu wengine ambao bado hawajakamatwa walikula njama ya ya kutenda makosa ya kughushi na ukwepaji wa Kodi.
Pia mshtakiwa Mwanyika (56), na Lugendo (46), wanadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.
Aidha washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Mei 16.2008 na Desemba 31,2008 huko Kahama na Biaramulo, walitoa tamko la uongo kwa kamishna Generali wa TRA kwa nia ya kukwepa kodi kulipa USD 9,309,600 ambayo ilikuwa ni kodi iliyopaswa kulipwa kwa TRA.
Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea, North Mara, exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika na Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo mwenye shati ya drafti akitoka katika mahakama ya hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kujibu tuhuma zinazomkabili.
Hivyo makala ALIYEKUWA RAIS WA MIGODI YA MADINI AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO
yaani makala yote ALIYEKUWA RAIS WA MIGODI YA MADINI AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ALIYEKUWA RAIS WA MIGODI YA MADINI AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/aliyekuwa-rais-wa-migodi-ya-madini.html
0 Response to "ALIYEKUWA RAIS WA MIGODI YA MADINI AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO"
Post a Comment