Loading...

BALOZI KARUME ASISITIZA UMOJA KULEA URITHI.

Loading...
BALOZI KARUME ASISITIZA UMOJA KULEA URITHI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BALOZI KARUME ASISITIZA UMOJA KULEA URITHI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BALOZI KARUME ASISITIZA UMOJA KULEA URITHI.
link : BALOZI KARUME ASISITIZA UMOJA KULEA URITHI.

soma pia


BALOZI KARUME ASISITIZA UMOJA KULEA URITHI.


Waziri wa Michezo Vijana Utamaduni na Sanaa Zanzibar Mhe. Balozi Ally Abeid Karume akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetakiwa kuendeleza umoja na mshikamano jambo ambalo litasaidia kulea urithi pamoja kutangaza vivutio vya utalii katika nchi mbalimbali duniani.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga Tamasha la Urithi wa Utamaduni Waziri wa Michezo Vijana Utamaduni na Sanaa Zanzibar Mhe. Balozi Ally Abeid Karume, amesema kuwa kufanyika kwa tamasha urithi ni jambo muhimu kwa taifa kwa  imesaidia  kuhamasisha watu mbalimbali kupenda tamaduni zao.

"Urithi wetu unapaswa tuendelee kulea, kitu ambacho tutajivunia na kuleta maendeleo katika kutangaza utamaduni wetu nchi mbalimbali" amesema Mhe. Balozi Karume.

Hata hivyo ameeleza kuwa licha ya changamoto za utamaduni wa kigeni, bado urithi wetu unapewa nafasi katika kuhakikisha watanzania wanakuwa na kumbukumbu za utamaduni wao.
Kikundi cha Ngoma ya asili kikitoa burudani baada ya mgeni rasmi wasili Waziri wa Michezo Vijana Utamaduni na Sanaa Zanzibar Mhe. Balozi Ally Abeid Karume katika kijiji cha Makumbusho leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabula akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabula, amesema kuwa tamasha la urithi wa utamaduni katika Mkoa wa Dar es Salaam limefanikiwa kwa asilimia kubwa.

Profesa Mabula amesema kuwa lengo la tamasha ni kuwavutia watalii wa ndani na nje  kuja kuangalia utamaduni wa urithi.

"Tanzania kuna vivutio vingi vya utalili ikiwemo malikale, zana za kale, magofu pamoja na magamoyo" amesema Profesa Mabula.
Utamaduni wa nyumba za Wasukuma ambayo ipo katika jijini cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Amesema Tanzania kuna utajiri mkubwa sana kutokana na vivutio vya utalii ambapo inaweza kuliingizia taifa pato kubwa.

Profesa Mabula amefafanua kuwa mpaka kufika mwaka 2020 Tanzania inatakiwa kuingiza watalii milioni mbili, lakini kwa mwaka wa jana tayari tuingiza watalii I,300,000 hapa nchini.

"Wizara wameona kuna utalii mwengine upo katika urithi wa utamaduni na sasa unafanyiwa kazi ili kuendelea kuwavutia watalii" amesema Profesa Mabula.

Katika hatua nyengine Profesa Mabula ameeleza kuwa baada ya kumalizika tamasha la urithi katika mkoa wa Dar es Salaam, Oktoba 9 hadi I3 mwaka huu watakuwa Mkoa Arusha kwa ajili ya tamasha la urithi.

"Mwaka huu tutafanya kwa baadhi ya mikoa, lakini mwakani itafanyika kila mkoa" amesema Profesa Mabula. 
Mratibu wa Maonyesho ya Jukwaa Mganga Mwanyenyelwa.
Mratibu wa Maonyesho ya Jukwaa Mganga Mwanyenyelwa, amesema kuwa  tamasha la urithi limekuwa la mafanikio tofauti na miaka ya nyuma.
Amesema kuwa wasanii wa fani mbalimbali wamepata fursa ya kushiriki ya kuonyesha sanaa pamoja na kuongeza idadi ya watalii.
"Wasanii wa fani za kiutamaduni wameweza kuonyesha na kuleza kwa kina ngoma za tamaduni za makabila mbalimbali hapa nchini" amesema Mwanyenyelwa.

Mwanyenyelwa amesema kuwa tamasha la mwaka huu limeshirikisha vikundi 43, ambapo vikundi hivyo vimepata fursa ya kushiriki kikamilifu na maonyesha sanaa za utamaduni.

Hata hivyo amefafanua kuwa katika tamasha lijalo wanatarajia kuongeza ubora kwa kutoa fursa ya vikundi bora kushiriki.

"Wadau mbalimbali wamekuwa na mwitikio mkubwa, kwani wamekuja idadi kubwa ya watu kuona maonyesho mbalimbali ya urithi, lakini mara ya mwisho kufanyika maonyesho haya ilikuwa mwaka I99I" amesema Mwanyenyelwa.


Hivyo makala BALOZI KARUME ASISITIZA UMOJA KULEA URITHI.

yaani makala yote BALOZI KARUME ASISITIZA UMOJA KULEA URITHI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI KARUME ASISITIZA UMOJA KULEA URITHI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/balozi-karume-asisitiza-umoja-kulea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BALOZI KARUME ASISITIZA UMOJA KULEA URITHI."

Post a Comment

Loading...