Loading...

BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU

Loading...
BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU
link : BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU

soma pia


BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Serikali Kuu kwa kushirikiana na Taasisi na Mashirika megine ya Kitaifa na Kimataifa kujenga Kituo cha Taifa kitakacholenga kuwahudumia Watu wenye ulemavu katika kuwajengea nguvu na maarifa ya kuendelea kujitegemea Kimaisha.

Alisema Ulimwengu wa sasa umebadilika kwa kubeba harakati nyingi zinazoibua matukio mbalimbali yanayosababisa Jamii kukumbwa na ajali tofauti  katokana na kasi ya maisha na hatimae kuzalisha Walemavu wanaohitaji huduma za matunzo na maarifa mengine ya Kimaisha.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla maalum ya kuzindua rasmi Kituo cha Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu cha Jimbo la Shaurimoyo kiliopo pembezoni mwa Skuli ya Sekondari ya Ufundi Mikunguni Mjini Zanzibar.

Alisema tabia ya kuwatenga Watu wenye Ulemavu haipendezi na nidhambi jambo ambalo halikubaliki katika Jamii yoyote ile. Hivyo aliwahimiza wahusika hao wasikubali kukata tamaa katika kupigania haki zao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushukuru Uongozi wa Kampuni ya Peny Royal na Kumpongeza Mwakilishi wa Jimbo la Shaurimoyo kwa jitihada zao zilizopelekea kujengwa kw kituo hicho muhimu kwa Watu wenye mahitaji Maalum.

Balozi Seif alifarajika kuona kwamba Ujenzi wa Kituo hicho umelenga kuwajengea Uwezo na maarifa Watu wenye Ulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo ili wawe Wajasiri Amali watakaokuwa na nguvu za kujiendesha wenyewe Kimaisha.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikizindua Rasmi Kituo cha Watu wenye Ulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo kilichojengwa pembezoni mwa Skuli ya Sekondari ya Ufundi Mikunguni Mjini Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud.
 Balozi Seif akiangalia na kufurahia bidhaa zinazozalishwa na Watu wenye Ulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo ndani ya Kituo kipwa alichokizindua rasmi.
 Mjumbe wa Kamati ya Mradi wa Kituo cha Watu wenye ulemavu cha Jimbo la Shaurimoyo Bibi Mrashi Mikidadi akiwasilisha Risala kwenye hafla ya uziduzi wa Kituo chao cha kazi za ujasiri amali pamoja na Ofisi.
 Balozi Seif akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Shaurimoyo katika hafla ya uziduzi wa Kituo chao cha kazi za ujasiri amali pamoja na Ofisi hapo pembezoni mwa Skuli ya Sekondari ya Ufundi Mikunguni.
 Balozi Seif akimkabidhi Baskeli Mtoto mwenyeulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo Feisal Mbarouk kwenye hafla ya uziduzi wa Kituo chao cha kazi za ujasiri amali pamoja na Ofisi hapo Mikunguni.
 - Mtoto Lutfia Mohamed ambae ni mlemavu akifurahia Baskeli mpya aliyokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi zilizotolewa na Wafadhili mbali mbali.
 Fundi Seremala wa Kituo cha Watu wenye ulemavu cha Jimbo la Shaurimoyo Bwana Juma Abdulaah Juma akipokea Baskeli yake itakayomsaidia katika harakati zake za Kimaisha. Picha na – OMPR –ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU

yaani makala yote BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/balozi-seif-azindua-kituo-cha-taifa-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU"

Post a Comment

Loading...