Loading...

BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA

Loading...
BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA
link : BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA

soma pia


BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA

Na.WFM Mjini Bali- Indonesia

Benki ya Dunia imeahidi kuwekeza zaidi nchini Tanzania katika Sayansi na Teknolojia ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa lengo la kuisaidia Tanzania kukuza uchumi wa viwanda na kuondoa umasikini kwa wananchi wa wake.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, alipofanya mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bw. Hafez Ghanem, katika mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Mjini Bali Indonesia.

Dkt. Mpango amesema kuwa Benki ya Dunia imeamua kuwekeza katika teknolojia kwa kuwa ni eneo sahihi linaloweza kukuza uchumi wa Taifa kwa zaidi ya mara mbili kutokana na tafiti zilizofanywa na Benki ya Dunia.

“Kimsingi Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia amefurahia ajenda za maendeleo za Tanzania kuhusu kujenga uwezo wa rasilimali watu katika kukuza uchumi wa viwanda na ameahidi kuanza kwa kuwekeza zaidi kwa watoto wenye umri mdogo ili mipango ya maendeleo ya nchi iwe endelevu”, alieleza Dkt. Mpango.

Aidha Waziri Mpango alimueleza Makamu wa Rais wa Benki hiyo kuwa Tanzania imeweka mikakati mbalimbali ya kujenga uchumi wa viwanda utakaotumia malighafi za ndani ili kuongeza ajira kwa wananchi walio wengi. 

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed, muda mfupi kabla ya Mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Bw. Hafez Ghanem, katika mkutano wa mwaka wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na WB, Mjini Bali Indonesia. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) akielezea miradi ya maendeleo ambayo inahitaji fedha ili iweze kuchochea uchumi ikiwemo miradi ya Nishati ya Umeme na ujenzi wa miundombinu ya Reli ya Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa – SGR alipofanya Mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Bw. Hafez Ghanem, katika mkutano wa mwaka wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na WB Mjini Bali Indonesia.

Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed(kulia) akizelezea miradi ya kukuza utalii ambayo inahitaji fedha ili kuweza kuchochea maendeleo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Bw. Hafez Ghanem, katika mkutano wa mwaka wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na WB, Mjini Bali Indonesia.

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Bw. Hafez Ghanem (katikati) akieleza nia ya Benki yake ya kuwekeza kwenye mafunzo ya Miradi ya pamoja kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma Mjini Bali Indonesia alipofanya Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani). (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango) .



Hivyo makala BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA

yaani makala yote BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/benki-ya-dunia-yaahidi-kutoa-fedha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUTOA FEDHA KUKUZA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA"

Post a Comment

Loading...