Loading...
title : Benki ya Exim Tanzania imejipanga kusaidia wakulima wa korosho mkoani Mtwara kwa msimu wa 2018
link : Benki ya Exim Tanzania imejipanga kusaidia wakulima wa korosho mkoani Mtwara kwa msimu wa 2018
Benki ya Exim Tanzania imejipanga kusaidia wakulima wa korosho mkoani Mtwara kwa msimu wa 2018
BENKI ya Exim Tanzania imejipanga kusaidia wakulima wa korosho mkoani Mtwara kwa uwekezaji wa shilingi milioni 200 ili kuongeza uzalishaji wakati wa msimu wa korosho wa 2018.
Sekta ya ulimaji wa korosho nchini Tanzania hivi karibuni imeshuhudia ukuaji wa kiasi kikubwa kwa kuongezeka uzalishaji na bei ya kuuza ambayo ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha maisha ya mkulima.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania Jafari Matundu, alisema katika mahojiano kwamba benki hiyo imekuwa ikisaidia wakulima na wasafirishaji wa korosho kwa miaka mingi kwa kuwapatia huduma mbalimbali za kifedha zilizo bora kabisa. "Tumekuwa mkoani Mtwara kwa miaka mingi sasa tukifanya kazi pamoja na wakulima na wasafirishaji wa korosho kwa kuwapa huduma za kisasa za kibenki kwa nia ya kusaidia kukuza biashara zao."
Benki ya Exim Tanzania ilifungua biashara mkoani Mtwara kusaidia wakulima wa korosho kwa sababu ni sehemu muhimu katika sekta ya kilimo nchini Tanzania. Kwa sasa, nchi inasafirisha korosho ghafi zaidi ya tani 350,000, ambayo ni ongezeko la karibu asilimia 100 kutoka miaka ya nyuma.
Benki ya Exim Tanzania imedhamiria kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania na kupanua biashara yao ili kufikia maeneo mengi zaidi nchini ili kuweza kutoa huduma za kibenki za kibunifu na muhimu kwa ajili ya kuimarisha shughuli za kilimo. Benki ya Exim hutoa huduma kwa wakulima kupitia Vyama vya Ushirika vya Kilimo na Masoko (AMCOS) Mtwara na Tandahimba. AMCOS ni jukwaa muhimu linalosaidia wakulima katika hatua za uzalishaji, usindikaji, usafirishaji na masoko wa mazao mbalimbali ya biashara ikiwa ni pamoja na korosho.
Mkurugezi Matundu aliongeza, "Kutokana na kuongezeka kwa bei za usafirishaji na uuzaji benki yetu iliona ni muhimu kuongeza uwekezaji kwenye kitabu cha mikopo ili kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa zao na hivyo kuongeza mapato yao kupitia mauzo yao. Wakulima wanahitaji usaidizi katika hatua zote za kilimo, kuanzia katika kuvuna, kununua mifuko, kulipa wafanyakazi hadi bidhaa kufikia mnunuzi.
Benki ya Exim imeadhimisha miaka 21 ya mafanikio katika ukuaji na uongozi katika masoko mapya barani Afrika. Benki ya Exim Tanzania ilianzishwa mwaka 1997 na kupanua soko lake kwa kufungua kampuni tanzu katika visiwa vya Komoro (2007), nchini Djibouti (2011) na Uganda (2016). Exim inajivunia kuwa benki kwanza kufungua matawi nje ya nchi. Lengo lake kuu ni kujenga thamani ya uwekezaji kwa wanahisa wake na kufikia ukuaji kupitia utoaji wa huduma za tofauti na zinazolenga mteja.
Hivyo makala Benki ya Exim Tanzania imejipanga kusaidia wakulima wa korosho mkoani Mtwara kwa msimu wa 2018
yaani makala yote Benki ya Exim Tanzania imejipanga kusaidia wakulima wa korosho mkoani Mtwara kwa msimu wa 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya Exim Tanzania imejipanga kusaidia wakulima wa korosho mkoani Mtwara kwa msimu wa 2018 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/benki-ya-exim-tanzania-imejipanga.html
0 Response to "Benki ya Exim Tanzania imejipanga kusaidia wakulima wa korosho mkoani Mtwara kwa msimu wa 2018"
Post a Comment