Loading...
title : BREAKING NEWZZZZ: WAZUNGU WAWILI WATAJWA KUHUSIKA MPANGO WA KUTEKWA KWA MO DEWJ
link : BREAKING NEWZZZZ: WAZUNGU WAWILI WATAJWA KUHUSIKA MPANGO WA KUTEKWA KWA MO DEWJ
BREAKING NEWZZZZ: WAZUNGU WAWILI WATAJWA KUHUSIKA MPANGO WA KUTEKWA KWA MO DEWJ
*Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar waanza msako kuhakikisha anapatikana
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuna Wazungu wawili wanatakwa kuhusika kuratibu mpango wa kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Mohemed Dewj 'Mo'.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa taarifa za awali zinaonesha tukio hilo kuna wazungu wawili wanahusika kuratibu tukio la kutekwa kwa Mo Dewj.
Kamanda Mambosasa amesema hayo asubuhi akiwa eneo la Hoteli ya Collessium jijini Dar es Salaam ambako tukio la kutekwa Mo linadaiwa kutokea."Tupa hapa kwa ajili ya kufuatilia tukio hili la kutekwa kwa Mo.Taarifa za awali ambazo tumezipata zinaonesha kuna Wazungu wawili wamehusika kuratibu tukio la Mo kutekwa.
"Tumeanza kufuatilia na wananchi wasiwe na wasiwasi,kikubwa watupe taarifa nasi tutazifanyia kazi," amesema Mambosasa.
KAULI YA MAKONDA
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema taarifa za kutekwa kwa Mo zimeshutua wengi lakini anaamini atapatikana kwani tayari vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi yake.Makonda amesema kuwa kikubwa wananchi wa Dar es Salaam kutokuwa na wasiwasi na wawe watulivu wakati vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufuatilia.
HAJJ MANARA ATOA NENO
Wakati huo huo Msemaji wa Klabu ya Simba Hajj Manara amesema kikubwa ni kwa sasa ni utulivu na kuacha vyombo vya ulinzi vifanye kazi yake.Pia amesema kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ni kumuomba ili Mo apatikane akiwa salama na anaamini atapatikana."Mbali ya kuwa Mo ni shabiki wa soka bado tukio la kutekwa kwake limeshutua makundi mbalimbali," amesema Manara.
Hivyo makala BREAKING NEWZZZZ: WAZUNGU WAWILI WATAJWA KUHUSIKA MPANGO WA KUTEKWA KWA MO DEWJ
yaani makala yote BREAKING NEWZZZZ: WAZUNGU WAWILI WATAJWA KUHUSIKA MPANGO WA KUTEKWA KWA MO DEWJ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BREAKING NEWZZZZ: WAZUNGU WAWILI WATAJWA KUHUSIKA MPANGO WA KUTEKWA KWA MO DEWJ mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/breaking-newzzzz-wazungu-wawili-watajwa.html
0 Response to "BREAKING NEWZZZZ: WAZUNGU WAWILI WATAJWA KUHUSIKA MPANGO WA KUTEKWA KWA MO DEWJ"
Post a Comment