Loading...

CHUO KIKUU KAMPALA CHATEKELEZA MAAGIZO YA TCU, CHAFANYA MABORESHO MAKUBWA.

Loading...
CHUO KIKUU KAMPALA CHATEKELEZA MAAGIZO YA TCU, CHAFANYA MABORESHO MAKUBWA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CHUO KIKUU KAMPALA CHATEKELEZA MAAGIZO YA TCU, CHAFANYA MABORESHO MAKUBWA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CHUO KIKUU KAMPALA CHATEKELEZA MAAGIZO YA TCU, CHAFANYA MABORESHO MAKUBWA.
link : CHUO KIKUU KAMPALA CHATEKELEZA MAAGIZO YA TCU, CHAFANYA MABORESHO MAKUBWA.

soma pia


CHUO KIKUU KAMPALA CHATEKELEZA MAAGIZO YA TCU, CHAFANYA MABORESHO MAKUBWA.


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala -Tanzania (KIUT) Profesa Jamidu Katima akizumgumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala- Tanzania (KIUT) kimefanya maboresho makubwa ya kiutendaji ikiwemo kuwaondoa wafanyakazi wasiokuwa na sifa jambo ambalo litasaidia kutoa elimu bora kwa wanafunzi wanaosoma chuo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Makamu Mkuu wa Chuo cha KIUT  Profesa Jamidu Katima, amesema kuwa chuo kimefanya maboresho makubwa ikiwemo kuwaondoa wafanyakazi wote wasiokuwana na sifa pamoja na kuwajiri wanataaluma 60.

Profesa Katima amesema kuwa wamepunguza idadi ya idara kutoka saba hadi kufika tatu pamoja na kuwaondoa wafanyakazi wote waliokuwa wanafanyakazi bila kuwa na vibali hapa nchini.

"Kwa kiasi kikubwa tumefanyia kazi mapungufu yaliyopelekea chuo kutokuruhusiwa kudahili, maeneo machache yaliyobaki tunaendelea kuyafanyia kazi" amesema Profesa Katima.
Baadhi ya majengo ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala-Tanzania (KIUT)
Hata hivyo amesema kuwa wanafunzi wanaoendelea na mwaka wa masomo katika Chuo hicho kwa 'allied health' wataanza Octoba 8, 20I8 na oktoba 29 wataanza program nyengine.
Katika hatua nyengine Profesa Katima, ameeleza kumekuwa na taarifa  ambazo sio sahihi kuhusu chuo cha KIUT baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kutoa taarifa.
Msomi huyo amefafanua kuwa TCU ilitolewa taarifa katika makundi matatu ambayo ni vyuo vilivyofungiwa, vyuo vinavyopaswa kuhamisha wanafunzi wanaondelea na masomo  na kutokuruhusiwa kudahili wanafunzi wapya.
"Chuo chetu kipo kwenye kundi la Tatu katika taarifa ya TCU ambapo tuanaendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wanaendelea na masomo kwa uangalizi, lakini haturuhusiwi kudahili wanafunzi wapya" amesema Profesa Katima.

Amesema kuwa vyema wazazi, walezi pamoja na wanafunzi wanaosoma chuo cha KIUT wasiwe na shaka yoyote badala yake waendelee na wamasoma.

Amesema kuwa mazingira ya Chuo yapo vizuri tunaendelea na masoma kwa ujumla.

Mwanafunzi wa Chuo Cha KIUT anayesoma Shahada ya Udaktari na Upasuaji latifa Abibu Mgala, amesema kuwa anajivunia kusoma chuo cha kampala kutokana elimu bora wanayopata kwa sasa.
Mwanafunzi wa Chuo Cha KIUT anayesoma Shahada ya Udaktari na Upasuaji latifa Abibu Mgala akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa walimu wanafundisha vizuri pamoja na kufanya mazoezi ya vitendo kwa wakati.

Waziri wa Elimu Serikali ya Wanafunzi katika Chuo Cha KIUT Samweli, amesema kuwa wanaendelea kutoa kusoma katika mazingira.
Amesema kuwa sasa chuo kimendelea kuyafanyia kazi mapungufu ndani ya chuo hicho jambo ambalo linawatia faraja kutokana huduma bora wanayopata.
Mazingira ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala -Tanzania.
Chuo Cha Kimataifa Cha Kampala-Tanzania mwaka 20I7 kilizuiliwa kudahili wanafunzi wapya kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyoainishwa na TCU.

Mwezi February mwaka huu, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa  Ndalichako akiwa na maafisa wa uhamiaji na TCU walitembelea chuo hicho na kubaini mapungufu ambayo kwa sasa yanafanyiwa kazi.

Machi mwaka huu chuo cha KIUT kilianza mchakato wa kufanya mabadiliko makubwa yakihusisha kuajiri watumishi waendeshaji, kupunguza idadi ya vitivo na idara, kuwaondoa wafanyakazi wasiokuwa na sifa.

Mabadiliko mengine ni kuwaondoa wafanyakazi waliokuwa hawana vibali vya kufanya kazi nchini pamoja na kuajiri wanataaluma ili kuziba mapengo na kupunguza idadi ya programu walizokuwa wanatoa.



Hivyo makala CHUO KIKUU KAMPALA CHATEKELEZA MAAGIZO YA TCU, CHAFANYA MABORESHO MAKUBWA.

yaani makala yote CHUO KIKUU KAMPALA CHATEKELEZA MAAGIZO YA TCU, CHAFANYA MABORESHO MAKUBWA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CHUO KIKUU KAMPALA CHATEKELEZA MAAGIZO YA TCU, CHAFANYA MABORESHO MAKUBWA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/chuo-kikuu-kampala-chatekeleza-maagizo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "CHUO KIKUU KAMPALA CHATEKELEZA MAAGIZO YA TCU, CHAFANYA MABORESHO MAKUBWA."

Post a Comment

Loading...