Loading...
title : DKT KALEMANI: AWATAKA MAMENEJA WA TANESCO NCHINI KUWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU KWENYE MAENEO YAO.
link : DKT KALEMANI: AWATAKA MAMENEJA WA TANESCO NCHINI KUWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU KWENYE MAENEO YAO.
DKT KALEMANI: AWATAKA MAMENEJA WA TANESCO NCHINI KUWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU KWENYE MAENEO YAO.
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza Mameneja wa shirika la Umeme (Tanesco) kote nchini kuhakikisha wanakata huduma ya umeme kwa wadaiwa sugu ikiwemo sekta binafasi na serikalini.
Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Morogoro iliyokuwa na lengo la kutembelea maeneo yanayozalisha umeme ikiwemo Kidatu ambako uzalishaji wa umeme ni 204 mw.
Licha ya kutembelea eneo hilo lakini pia alizindua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Alisema kwamba hatua hiyo inaweza kuwa mwarobaini wa kuweza kusaidia kukusanya madeni hayo ambayo yamekuwa kwa muda mrefu na hivyo kupelekea kukwamisha malengo yao waliojiwekea.
Aidha alisema kwamba haiwezekani shirika hilo likawa linawadai watu fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwenye kutekeleza shughuli za kimaendeleo na kuweza kuwafikia wananchi wengi huku wakiacha kuwachukulia hatua ambazo zinaweza kusaidia kupata ufumbuzi wake.
“Ndugu zangu mameneja wa mikoa hakikisheni mnawakatia umeme wadaiwa wote sugu kwenye maeneo yenu wakiwemo wale wa sekta binafasi na serikali kwani hii ndio njia inayoweza kuwasaidia kukusanya madeni hayo “Alisema Dkt Kalemani. Akizungumzia kitengo cha huduma kwa wateja ndani ya shirika hilo Dkt Kalemani alisema ni muhimu watumishi wa kada hiyo wakabadilikana kitabia kwa sababu imedodira sana na kwenye maeneo mengi hazifanyi kazi zao ipasavyo.
Hivyo makala DKT KALEMANI: AWATAKA MAMENEJA WA TANESCO NCHINI KUWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU KWENYE MAENEO YAO.
yaani makala yote DKT KALEMANI: AWATAKA MAMENEJA WA TANESCO NCHINI KUWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU KWENYE MAENEO YAO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT KALEMANI: AWATAKA MAMENEJA WA TANESCO NCHINI KUWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU KWENYE MAENEO YAO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/dkt-kalemani-awataka-mameneja-wa.html
0 Response to "DKT KALEMANI: AWATAKA MAMENEJA WA TANESCO NCHINI KUWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU KWENYE MAENEO YAO."
Post a Comment