Loading...
title : DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO
link : DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO
DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO
Na Mathias Canal-WK, Mseke-Iringa
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), amewataka wakulima wa nyanya Mkoani Iringa kuchangamkia fursa ya kuongeza uzalishaji wa nyanya ili kuakisi uhitaji wa viwanda vya nyanya ikiwa ni pamoja na kiwanda cha Darsh chenye uwezo wa kusindika Tani 250 za nyanya kwa siku.
Waziri Tizeba ametoa mwito huo jana Octoba 18, 2018 wakati akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Kiwanda hicho kinafanya shughuli za ukusanyaji wa nyanya kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa na mikoa ya jirani na kufanya usindikaji wa nyanya ambapo hupeleka kiwanda cha Arusha kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na nyanya ambazo huuzwa ndani na nje ya nchi.
Waziri Tizeba, aliwataka wakulima hao kujiunga kuanzisha kikundi cha ushirika ili kuwa na urahisi wa mikopo ili kuwezesha uwezo wa uwekezaji kupitia kilimo cha umwagiliaji kitakachoongeza tija katika kipato chao na jamii kwa ujumla.“Wakulima wa nyanya hapa Igwachanya na hata katika maeneo mengi nchini wanalima kwa kutegemea mvua na uzalishaji huwa mdogo na usiokidhi mahitaji ya soko hivyo nawasihi kuongeza uzalishaji wa nyanya kwani soko la uhakika lipo” Alikaririwa Dkt Tizeba
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mtambo wa kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018. Mwingine Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakifatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), alipotembelea na kukagua kiwanda cha Darsh jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
aziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Hivyo makala DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO
yaani makala yote DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/dkt-tizeba-awataka-wakulima-wa-nyanya_54.html
0 Response to "DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO"
Post a Comment