Loading...

HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE

Loading...
HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE
link : HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE

soma pia


HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amemtaka mkandarasi  Makapo Contractors and General Supplies co. Ltd anayejenga barabara ya Masasi-Mpeta KM 16 na Dott Service Limited anayejenga barabara ya Mtwara- Mlivata KM 50 kukamilisha barabara hizo kwa wakati.
Amesema  kuanzia sasa Serikali haitakuwa na muda wa kumwongezea mkandarasi atakayebainika amechelewesha ujenzi kinyume cha mkataba.
“Nimeridhika na ubora wa kazi yenu ni nzuri ila ongezeni kasi ili manufaa ya kuwepo kwa barabara ya lami kwa wananchi wa Mtwara yalete matokeo chanya haraka”, amesema Mhandisi Kamwelwe.
Amesema  barabara ya Masasi-Mpeta KM 16 na Mtwara- Mlivata KM 50 ni sehemu ya barabara kuu ya uchumi Mkoani Mtwara yenye urefu wa KM 210 inayoanzia Mtwara mjini kupitia Mlivata, Nanyamba,Tandahimba, Newala hadi Masasi.
“barabara hii ikikamilika kwa wakati itaufungua uchumi wa wakazi wa Mtwara kwa kuongeza fursa za ajira, kilimo na biashara”, amesisitiza Mhandisi Kamwelwe .
Naye mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw, Evod Mmanda ameishukuru serikali kwa kasi yake katika ujenzi wa barabara hiyo ambayo ikikamilika itachochea utekelezaji wa sera ya viwanda, utalii, kilimo  na uvuvi na hivyo kuzalisha fursa nyingi za ajira kwa wananchi.
“Tumejipanga kuhakikisha tunashirikiana na mkandarasi  MAKAPO na DOTT ili kazi zao ziende kwa haraka na kuiwezesha Serikali kuendelea kujenga barabara za lami katika maeneo ya Nanyamba,Tandahimba,Newala na hivyo kuuunganisha kwa lami mkoa wa Mtwara na wilaya zake.
Waziri wa Mhandisi Kamwelwe yuko mkoani Mtwara kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano na kuhimiza kasi ya ujenzi.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumzana wananchi wa Tunduru mkoani Ruvuma mara baada ya kukagua eneo la njia panda mjini humo na kuahidi ujenzi wa barabara ya mchepuo ili kupunguza msongamano na ajali (katikati), ni Mbunge wa Tunduru Mhandisi, Ramo Makani.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akisisitiza jambo kwa mkandarasi Dott anayejenga barabara ya Mtwara-Mlivata KM 50 mara baada ya kuikagua (kulia), kwake ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mtwara Mhandisi John Chacha na kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw, Evod Mmanda. 
Muonekano wa barabara ya Mtwara-Mlivata KM 50 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani Mtwara.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto na Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Mkoa wa Mtwara Mhandisi John Chacha wakikagua ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mlivata KM 50 inayojengwa na kampuni ya Dott. 
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO




Hivyo makala HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE

yaani makala yote HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/hatutaongeza-muda-wa-ujenzi-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE"

Post a Comment

Loading...