Loading...

JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI

Loading...
JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI
link : JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI

soma pia


JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI

Na Lydia Churi- Mahakama, Mwanza
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka watumishi wa Mahakama katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza hususan Mahakimu kutimiza wajibu wao kikamilifu kwa kuhakikisha wanamaliza kesi ili wananchi waweze kupata haki kwa wakati.
Akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nansio-Ukerewe pamoja na Mahakama za Mwanzo za Ilangala na Nansio mjini, Jaji Mkuu pia amewakumbusha Mahakimu kuhakikisha hukumu zinatolewa ndani ya siku 90 baada ya shauri kusikilizwa na endapo siku zitazidi basi zisizidi siku ishirini na moja.
Alisema Mahakama ya Tanzania inafanya kila jitihada ili kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati huku akitolea mfano wa nakala za hukumu kutolewa bure. Alisema Mahakama imeingia mkataba na shirika la Posta ili kusambaza nakala za hukumu pamoja na nyaraka nyingine za mahakama.
“Suala la hakimu kuchelewesha hukumu bila sababu za msingi halikubaliki na ni utovu wa nidhamu, jiwekeni kwenye nafasi ya wanaocheleweshewa hukumu ndipo mtaona ni kwa namna gani wanaumizwa na suala hili”, alisema Jaji Mkuu.
Awali akizungumza na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukererwe Bwana Focus Majumbi, Jaji Mkuu alitoa wito kwa viongozi wa serikali kusaidia kuwaelimisha wananchi taratibu za Mahakama ili wapate haki kwa wakati kwa kuwa haki ni kwa mujibu wa Sheria.
Alisema wananchi wengi hawafahamu taratibu za Mahakama ambapo badala ya kudai haki zao Mahakamani huenda kwa watu wasiohusika na kusababisha haki zao kuchelewa.
Naye Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukerewe aliiomba Mahakama ya Tanzania kuanza kuitumia Mahakama ya Mwanzo ya Irugwa ambayo hivi sasa haijaanza kutumika kutokana na ukosefu  watumishi. Mkuu huyo wa wilaya pia aliiomba Mahakama kusaidia ili wilaya yake isaidiwe kupata Mwenyekiti wa kudumu wa mabaraza ya kata.
Jaji Mkuu wa Tanzania anaendelea na ziara yake ya siku nne mkoani Mwanza ambapo atakagua utekelezaji wa shughuli za Mahakama.


Hivyo makala JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI

yaani makala yote JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/jaji-mkuu-ataka-kesi-zimalizike-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI"

Post a Comment

Loading...