Loading...
title : JESHI LA POLISI LATOA RAI KWA WAZAZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO
link : JESHI LA POLISI LATOA RAI KWA WAZAZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO
JESHI LA POLISI LATOA RAI KWA WAZAZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa rai kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao wadogo ikiwa ni pamoja na kuwawekea uangalizi mzuri kwa muda wote ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapa watoto hao pindi wanapokuwa wenyewe.
Kwa kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya watoto kuanzia umri wa miaka 03 hadi 12 kufariki kutokana na kutumbukia katika visima vya maji, katika mabwawa ya maji au katika mito pindi wanapovuka kuelekea Shuleni.
Kuelekea msimu wa mvua ambazo kwa baadhi ya maeneo tayari zimeanza kunyesha na kuleta madhara kwa binadamu. Yapo mambo ya kuepuka hasa matumizi ya vifaa vya umeme kama vile redio, tv na simu za mkononi wakati mvua kubwa zinazoambatana na radi zikinyesha.
Kwa Mkoa wa Mbeya mvua zilizonyesha maeneo ya Kyela na Mbalizi zimesababisha vifo vya watu watatu ambao walifariki dunia kwa kupigwa radi huku mmoja kati yao alipigwa na radi wakati akisikiliza radio.
Pia tunatoa angalizo kwa watu wanaofanya shughuli za uchimbaji madini katika migodi, kuchukua tahadhari za kiusalama ili kuepuka ajali katika maeneo hayo hasa za kuangukiwa vifusi vya udongo hususani msimu wa mvua. Tunapaswa kuchukua tahadhari kwa kufukia mashimo yasiyokuwa na dhahabu kwani ni hatari kwa watoto na watu wazima pindi wanapojaa maji.
Ni wito wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ulinzi wa mtoto, malezi bora kwa mtoto na pia kuwasaidia watoto hasa kuwavusha katika maeneo yenye mito au maji mengi ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapata. Pia ni kipindi cha kufukia mashimo, madimbwi yenye maji kwa ni hatari hasa kuelekea msimu wa mvua.
Imetolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.
Hivyo makala JESHI LA POLISI LATOA RAI KWA WAZAZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO
yaani makala yote JESHI LA POLISI LATOA RAI KWA WAZAZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JESHI LA POLISI LATOA RAI KWA WAZAZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/jeshi-la-polisi-latoa-rai-kwa-wazazi.html
0 Response to "JESHI LA POLISI LATOA RAI KWA WAZAZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO"
Post a Comment