Loading...
title : JETI YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI JUU YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI
link : JETI YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI JUU YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI
JETI YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI JUU YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI
Na Said Mwishehe,Flobu ya jamii
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini(JET)kimeamua kuwajengea uelewa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu uhifadhi wa mazingira na wanyamapori nchini
Akizungumzia semina hiyo inayofanyika wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Mkurugenzi Mtendaji John Chikomo amefafanua lengo kubwa la mafunzo ni kuwajengea uelewa waandishi hao kuhusu sekta yenyewe na kuhamasisha uhifadhi wa wanyamapori.
Pia amesema lengo lingine la semina hiyo ni kutangaza utalii wa ndani ili uweze kueleweka kimataifa na kuwashawishi sekta binafsi kuwekeza kwenye uhifadhi na utalii.
Chikomo amefafanua ni matarajio yao baada ya mafunzo hayo waandishi watakuwa na uelewa mpana kuhusu uhifadhi wa mazingira na wanayama pori na baada ya semina hiyo waandishi watapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo kwa kutembelea hifafhi za wanyamapori.
"Tumeanza na mafunzo haya na baadae tutaendelea na hatua nyingine zinazofuata ikiwemo ya waandishi husika kwenda kufanya uchunguzi kwa kuandika habari zinazohusu mazingira na uhifadhi.
" Mafunzo haya ni sehemu ya mradi unaoshughulikia kuendeleza uhifadhi mazingira ambapo ndani yake pamoja na kuangalia mafanikio pia unashughulika na changamoto zinazohusu uhifadhi,"amesema.
Wakati huo huo baadhi ya watoa mada wameeleza kwa kina kuhusu historia ya uhifadhi wa wanyamapori na mazingira pamoja na sheria mbalimbali zilizopo kwa nyakati tofauti na namna ambavyo zinafanyakazi nchini.
Mmoja wa watoa mada Stanslaus Nyambea kutoka Timu ya Wanasheria wabobezi kwenye masuala ya mazingira( LEAT) amezungumzia sheria ya fidia kwa watu wanaopata madhara kutoka kwa wanyama aidha iwe kwa kusababisha kifo au kuharibu mali ambapo sheria hiyo inaonekana kuwa na mlolongo mrefu wa kupata fidia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini(JET) John Chikomo akifafanua jambo kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sekta ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina ya mafunzo ya waandishi wa habari za mazingira.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) wa kwanza kushoto pamoja na waandishi wengine wa vyombo vya habari wakisikiliza mada kwenye semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi kuhusu sekta ya uhifadhi wa wanyamapori.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) na watoa mada.
Hivyo makala JETI YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI JUU YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI
yaani makala yote JETI YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI JUU YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JETI YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI JUU YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/jeti-yawajengea-uwezo-waandishi-juu-ya.html
0 Response to "JETI YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI JUU YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI"
Post a Comment