Loading...
title : KUKANDA ASHUSHA RUNGU KWA WALIMU WATATU WA SHULE ZA MSINGI ZILIZOSHIKA NAFASI ZA MWISHO KITAIFA KUTOKA IGUNGA
link : KUKANDA ASHUSHA RUNGU KWA WALIMU WATATU WA SHULE ZA MSINGI ZILIZOSHIKA NAFASI ZA MWISHO KITAIFA KUTOKA IGUNGA
KUKANDA ASHUSHA RUNGU KWA WALIMU WATATU WA SHULE ZA MSINGI ZILIZOSHIKA NAFASI ZA MWISHO KITAIFA KUTOKA IGUNGA
Na TIGANYA VINCENT
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Joseph Kakunda ameagiza kuvuliwa wadhifa wake Afisa Elimu Kata ya Malagano Wilayani Igunga Raphael Kapela kwa kusema hawezi kuhamia kwenye kituo chake cha kazi kwa sababu ya kuwa na familia kubwa inayomtegemea.
Alisema kitendo cha Afisa huyo kuishi Nkinga badala ya Malagano kumesababisha Shule ya Msingi Malagano kufanya vibaya katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi ya darasa la saba mwaka huu.
Kakunda alichukua hatua hiyo wilayani Igunga wakati wa ziara yake ya kutembelea shule mbili za Shule ya Msingi zilizofanya vibaya na kisha kutembelea Shule ya Sekondari ya Bukoko ambayo Hosteli yake iliungua moto.
Alisema kuwa Afisa huyo kwa kitendo cha kusema kuwa hawezi kuishi Malagano kwa sababu hakuna nyumba za kuishi watumishi na kwa sababu pia ana familia kubwa kinaonyesha kuwa hatoshi kushika nafasi hiyo.
Kakunda alisema kuwa nafasi hiyo ichukuliwe na mtu mwingine ambaye atakuwa tayari kuishi Malagano hata kama ni nyumba ya nyasi ili aweze kusimamia maendeleo ya elimu na nidhamu ya walimu katika Shule hiyo ili isifanye vibaya tena.
Alisema kitendo cha Mtumishi kukaa sehemu kwa sababu ya kuwepo kwa nyumba ya nyasi hakiwezi kuwa kinga na uhalali kwake kuishi mbali na kituo chake cha kazi kwa sababu kinapunguza ufanisi katika kutekeleza majukumu yake.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Joseph Kakunda akiongeza na baadhi ya Viongozi na wanakijiji alipotembelea Shule ya Msingi Mwazizi kufuatilia kwanini ilifanya shule hiyo ilifanya vibaya katika mtihani wa kumaliza la saba na kuwa ya pili kutoka mwisho kitaifa.
Mwalimi Mkuu wa Shule ya Msingi Mwazizi wilayani Igunga Musa Kitenya akisoma taarifa inayoonyesha sababu za kufanya vibaya kwa shule yake katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na kuifanya kuwa ya pili kutoka mwisho kitaifa.
Baadhi ya Viongozi na wanakijiji wa Kijiji cha Mwazizi wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (hauyopo kwenye picha) wakati alipotembelea Shule ya Msingi Malagano kufuatilia kwanini ilifanya shule hiyo ilifanya vibaya katika mtihani wa kumaliza la saba na kuwa ya pili kutoka mwisho kitaifa.
Hivyo makala KUKANDA ASHUSHA RUNGU KWA WALIMU WATATU WA SHULE ZA MSINGI ZILIZOSHIKA NAFASI ZA MWISHO KITAIFA KUTOKA IGUNGA
yaani makala yote KUKANDA ASHUSHA RUNGU KWA WALIMU WATATU WA SHULE ZA MSINGI ZILIZOSHIKA NAFASI ZA MWISHO KITAIFA KUTOKA IGUNGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUKANDA ASHUSHA RUNGU KWA WALIMU WATATU WA SHULE ZA MSINGI ZILIZOSHIKA NAFASI ZA MWISHO KITAIFA KUTOKA IGUNGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/kukanda-ashusha-rungu-kwa-walimu-watatu.html
0 Response to "KUKANDA ASHUSHA RUNGU KWA WALIMU WATATU WA SHULE ZA MSINGI ZILIZOSHIKA NAFASI ZA MWISHO KITAIFA KUTOKA IGUNGA"
Post a Comment