Loading...

MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA

Loading...
MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA
link : MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA

soma pia


MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA


Na Aisha Abdallah, Mahakama Kuu Tabora

Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole amefungua rasmi Mafunzo ya Mahakimu na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata mkoani humo yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuyasimamia mabaraza ya kata katika utekelezaji wa majukumu kwa mujibu wa sheria.

Akifungua Mafunzo hayo mapema Oktoba 08, katika Ukumbi wa Katibu Tawala, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Bongole aliwaelezea washiriki wa mafunzo hayo kuwa ni muhimu kwa sababu yataleta uelewa wa pamoja kati ya Mahakama na Mabaraza ya Kata juu ya mamlaka ya Mahakama na Mabaraza katika utoaji haki.

Aidha katika hotuba yake ya ufunguzi,Mhe. Jaji Mfawidhi huyo pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa kumsikiliza mtu kabla ya kutoa maamuzi na kuwaasa wanasemina kuyatekeleza mambo yote watakayojifunza katika semina hiyo. “Kama sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama suala la ushirikishwaji wa Wadau limepewa kipaumbele ili tuweze kufanikisha huduma ya utoaji haki”, alisema Mhe. Jaji Bongole.

Katika semina hiyo, Mahakama imewashirikisha Wanasheria kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora na Halmashauri ya Manispaa-Tabora kama viongozi wa Mabaraza ya Kata. Mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania na kuendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).

Washiriki ni Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo kutoka Tabora Mjini, Urambo, Nzega na Igunga pamoja na wajumbe wa Mabaraza ya
Kata na Wanasheria wa Halmashauri ya Manispaa na wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora


Sehemu ya Washiriki wakiwa katika Mafunzo hayo. 
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata wanaoshiriki katika Mafunzo ya siku tatu, Oktoba 08, 2018 hadi Oktoba, 10, 2018. 
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole  (katikati) ambaye pia alikuwa Mhe. Mgeni rasmi wa Mafunzo hayo, akiwa katika picha ya pamoja na Wanasheria wa Manispaa ya Tabora (waliosimama). 


Hivyo makala MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA

yaani makala yote MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/mafunzo-yatolewa-kwa-mahakama-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA"

Post a Comment

Loading...