Loading...

MRADI WA STIEGLER’S UTASADIA KUTUNZA MAZINGIRA - MAJALIWA

Loading...
MRADI WA STIEGLER’S UTASADIA KUTUNZA MAZINGIRA - MAJALIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MRADI WA STIEGLER’S UTASADIA KUTUNZA MAZINGIRA - MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MRADI WA STIEGLER’S UTASADIA KUTUNZA MAZINGIRA - MAJALIWA
link : MRADI WA STIEGLER’S UTASADIA KUTUNZA MAZINGIRA - MAJALIWA

soma pia


MRADI WA STIEGLER’S UTASADIA KUTUNZA MAZINGIRA - MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano wa kujenga mradi wa kuzalisha umeme kwenye maporomoko ya mto Rufiji, Stiegler’s Gorge utasaidia sana kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo utakapojengwa mradi huo, leo (Alhamisi, Oktoba 4, 2018), Waziri Mkuu amesema umeme utakaotokana na maji, utazalishwa kwa gharama nafuu na utakuwa wa uhakika zaidi.

Amesema kwa vile umeme utakaozalishwa katika mradi wa Stiegler’s Gorge utakuwa wa bei nafuu na hivyo kuwa rafiki kwa wananchi wa kipato cha chini, utatumika kama nishati mbadala kwa kuni na mkaa  ambao umechangia sana kwenye uharibifu wa mazingira hasa ukataji miti.

Waziri Mkuu Majaliwa amewaomba viongozi wa Serikali na vyama vya siasa wawaelimishe Watanzania kuwa mradi wa Stiegler’s Gorge una faida kubwa kwa Taifa kiuchumi na hauna athari za mazingira na badala yake utayaboresha.

Amewahakikishia Watanzania kuwa mradi huo utajengwa na utakamilika katika muda uliokusudiwa ambao ni miezi 36 kuanzia siku mkandarasi atakapokabidhiwa kazi hiyo.

Akizungumzia usalama katika eneo la mradi, Waziri Mkuu amesema viongozi wa mikoa ya Morogoro na Pwani wahakikishe kwamba wanaweka ulinzi wa kutosha kuanzia sasa na wakati  ujenzi utakapoanza ili kuzuia hujuma  na vitendo vya wizi na udokozi vinavyoweza kuvuruga kasi ya ujenzi wa mradi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo lililoandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kuzalisha Umeme katika Maporomoko ya Mto Rufiji- Stieglers Gorge wakati alipotembelea eneo hilo Oktoba 4, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani. 
Eneo litakapojengwa tuta la kukinga maji katika Mradi wa Kuzalisha Umeme  kwenye Maporomoko ya Mto Rufiji- Stieglers Gorge ambalo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilitembelea, Oktoba 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa tawi la reli litakalounganisha Stesheni ya Fuga katika reli ya TAZARA na eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme wa Moporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge wakati alipotembelea Stesheni hiyo, Oktoba 4, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA, Fuad Abdallah.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka wa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) kuhusu ujenzi wa tawi la reli litakalounganisha Stesheni ya Fuga katika reli ya TAZARA na eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme wa Maporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge wakati alipotembelea eno hilo Oktoba 4, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA, Fuad Abdallah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Moporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge, Oktoba 4, 2018.



Hivyo makala MRADI WA STIEGLER’S UTASADIA KUTUNZA MAZINGIRA - MAJALIWA

yaani makala yote MRADI WA STIEGLER’S UTASADIA KUTUNZA MAZINGIRA - MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MRADI WA STIEGLER’S UTASADIA KUTUNZA MAZINGIRA - MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/mradi-wa-stieglers-utasadia-kutunza.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MRADI WA STIEGLER’S UTASADIA KUTUNZA MAZINGIRA - MAJALIWA"

Post a Comment

Loading...