Loading...

MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi zote 16 za SADC

Loading...
MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi zote 16 za SADC - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi zote 16 za SADC, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi zote 16 za SADC
link : MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi zote 16 za SADC

soma pia


MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi zote 16 za SADC

Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu wamesaini mkataba wa makubaliano ya MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

Hatua hii inafuatia uteuzi wa serikali ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ulifanywa wakati wa mkutano wa SADC wa mawaziri wa Afya wa nchi wanachama, uliofanyika mwezi Novemba, 2017 nchini Afrika Kusini. 
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Bwanakunu amesema tangu wakati huo hadi sasa wamekuwa wakishirikiana na na Sekretarieti ya (SADC) kuandaa rasimu ya mpango wa utekelezaji wa manunuzi ya pamoja yaani SADC Pooled Procurement Services (SPPS). 

 Amesema kulingana na mpango huo, uratibu wa manunuzi unaanza rasmi tarehe leo, tarehe 9/10/2018, kupitia mkataba wa makubaliano yaani Memorandum of Understanding (MoU) kati ya MSD na Sekretarieti ya SADC. 
 Bwanakunu ameongeza kuwa MSD itakuwa na majukumu ya kupokea mahitaji ya manunuzi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutoka kwa nchi hizo 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, kusimamia takwimu na taarifa za dawa pamoja na kusimamia Kanzidata (Database) ya dawa za nchi hizo. 

 Ameongeza kuwa MSD itasimamia bei elekezi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, kusimamia mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao kwa nchi zote wanachama, kutoa huduma za kitaalam na kupanga bei elekezi. MSD pia itaanzisha kitengo maalumu ndani ya kurugenzi ya manunuzi kwa ajili ya kazi hii ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba ba vitendanishi vya maabara kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC tu. 

 Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax ameeleza kuwa Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa dawa kwa nchi za Ukanda wa SADC ni heshima kubwa kwa Taifa, kuaminiwa kwa huduma bora, uwezo na kukidhi vigezo vya kitaalamu katika mnyororo wa ugavi. 

 Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye amesema kwamba SADC imeipa Tanzania heshima kubwa na kuichagiza MSD kuhakikisha inatekeleza majukumu yake vizuri ili isionekane kuwa SADC ilifanya makosa kuichagua Tanzania.
Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu wakisaini mkataba wa makubaliano ya MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) makao makuu ya MSD jijini Dar es salaam Oktoba 9, 2018
Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini  mkataba wa makubaliano ya MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) makao makuu ya MSD jijini Dar es salaam Oktoba 9, 2018 
Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu wakionesha nyaraka za mkataba wa makubaliano ya MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) makao makuu ya MSD jijini Dar es salaam Oktoba 9, 2018
Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu baada ya hafla hiyo fupi makao makuu ya MSD jijini Dar es salaam Oktoba 9, 2018


Hivyo makala MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi zote 16 za SADC

yaani makala yote MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi zote 16 za SADC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi zote 16 za SADC mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/msd-kuwa-mnunuzi-mkuu-wa-dawa-vifaa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi zote 16 za SADC"

Post a Comment

Loading...