Loading...
title : NACSAP III IMEONGEA MAGEUZI YA UTENDAJI WA TAKUKURU
link : NACSAP III IMEONGEA MAGEUZI YA UTENDAJI WA TAKUKURU
NACSAP III IMEONGEA MAGEUZI YA UTENDAJI WA TAKUKURU
Na Ismail Ngayonga,MAELEZO
DAR ES SALAAM
UTAWALA Bora ni kipaumbele cha msingi katika Serikali yoyote duniani katika kufikia malengo ya Maendeleo ya Taifa ikiwa ni pamoja na kukuza na kuimarisha amani, utulivu, ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na kupunguza umaskini.
Dhana ya Utawala bora imeendelea kusisitizwa na kuimarishwa katika Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutekeleza maboresho mbalimbali katika Sekta ya Umma ili kukuza uwajibikaji, uwazi na uadilifu katika matumizi ya rasilimali za umma.
Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji (NACSAP) ni moja ya maboresho ya Sekta ya Umma ambao ulitekelezwa katika awamu mbili ya miaka 10 (2001 -2011) ikiwa ni juhudi za Serikali za kuunga mkono mapambano dhidi ya rushwa ili kuimarisha utawala bora katika sekta zote za uchumi.
Awamu ya Tatu ya Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa (2017-2022) imeandaliwa ikiwa na mtizamo mpya unaolenga kuhakikisha kuwa rushwa inaondolewa nchini kwa kutumia mbinu mpya na zinazotekelezeka kwa kuweka mkazo katika sekta zenye mazingira shawishi ya rushwa.
Utekelezaji wa Mkakati wa Awamu ya Tatu unalenga kupunguza na kudhibiti rushwa katika Sekta/maeneo muhimu ya kimkakati ambayo ni pamoja na manunuzi ya umma, ukusanyaji wa mapato, utoaji wa haki, maliasili na utalii, madini, nishati, mafuta na gesi, afya, elimu na ardhi.
Uratibu wa utekelezaji wa Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa Awamu ya Tatu utafanyika ndani ya muundo wa Serikali uliopo kuanzia ngazi ya Kijiji, Mtaa hadi Taifa kupitia Kamati za Kudhibiti Uadilifu na Kamati za Uratibu wa Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa.
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika anasema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.
Kutokana na jitihada za TAKUKURU na wadau wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, tatizo la Rushwa limepungua kiasi katika nchi yetu katika upimaji wa hali ya rushwa uliofanywa na Mashirika ya Kimataifa ambao umeonesha Tanzania kufanya vizuri miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki ikishika nafasi ya pili baada ya Rwanda.
Waziri Mkuchika anasema katika kipindi cha mwezi Julai, 2017 hadi Machi, 2018 Uchunguzi wa majalada 325 ulikamilika na kuwasilishwa kwa Mkurugenziwa Mashtaka kuombewa kibali, ambapo Majalada 214 yaliyopelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka yalipata kibali cha kuwafikisha watuhumiwa mahakamani.
“Kesi 219 ziliamuliwa mahakamani ambapo kesi 81 watuhumiwa wake waliachiwa huru na kesi 138 watuhumiwa wake walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo au kulipa faini, kesi14 ziliondolewa mahakamani kutokana na sababu mbalimbali na kesi 494 zinaendelea mahakamani” anasema Waziri Mkuchika.
Aidha anaongeza kuwa katika kuimarisha mifumo ya udhibiti wa mianya ya rushwa katika maeneo ya kodi na ukusanyaji mapato na manunuzi, Serikali ilianzisha utaratibu wa matumizi ya Mashine za Kielekroniki katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na tathmini ya hali ya rushwa katika utekelezaji wa Sheria ya Manunuzi ngazi ya Serikali za Mitaa katika Sekta ya Elimu na Afya.
Akifafanyua zaidi anasema jumla ya Kazi 329 za uchambuzi wa mifumo na Warsha 179 vya wadau zilifanyika kwa ya kujadili matokeo ya kazi za utafiti na uchambuzi wa mifumo hiyo ili kuweka mikakati ya kudhibiti rushwa vilifanyika katika Sekta 24 ambapo kazi 73 za ufuatiliaji wa utekelezaji wa maazimio yatokanayo na mapendekezo ya uchambuzi wa mifumo hiyo zilifanyika.
Katika eneo la miradi ya Maendeleo, Waziri Mkuchika anasema jumla ya Miradi ya maendeleo 195 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 154 ilifuatiliwa katika Sekta za Elimu, Afya, Maji na Ujenzi ili kuhakikisha kuwa fedha za umma zinatumika kama zilivyokusudiwa na thamani ya fedha inapatikana.
“Katika ufuatiliaji huu miradi 73 yenye thamani ya Shilingi bilioni 30.9 ilibainika kuwa na mapungufu katika utekelezaji wake na Uchunguzi umeanzishwa kwenye miradi 31 yenye thamani ya Shilingi bilioni 10” anasema Waziri Mkuchika.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika anasema kufuatia kasoro zilizojitokeza katika baadhi ya miradi, TAKUKURU ilipendekeza wasimamizi wa miradi 13 wachukuliwe hatua za kinidhamu na mamlaka kutokana na kasoro zilizobainika katika miradi waliyoisimamia.
Waziri Mkuchika anasema kiasi cha Tsh. Bilioni 58.4 ziliokolewa kutokana na operesheni zilizofanywa na TAKUKURU na kurejeshwa Serikalini kutokana na kudhibiti rushwa katika eneo la ukusanyaji mapato ya Serikali, uzuiaji wa malipo hewa na ukaguzi wa miradi ya Maendeleo.
Rushwa ni janga ambalo lina athari hasi katika jamii, inadhoofisha ustawi wa demokrasia katika nchi, ukiukwaji wa haki za binadamu, inasababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii na kuchelewesha maendeleo ya nchi.
Ili kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi, ni wajibu wa Viongozi wa Serikali katika ngazi zote, AZAKI, Sekta Binafsi na Wananchi kwa ujumla kuzingatia misingi ya uwazi na uwajibikaji Tatu katika Taasisi zao na Taifa kwa ujumla.
Hivyo makala NACSAP III IMEONGEA MAGEUZI YA UTENDAJI WA TAKUKURU
yaani makala yote NACSAP III IMEONGEA MAGEUZI YA UTENDAJI WA TAKUKURU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NACSAP III IMEONGEA MAGEUZI YA UTENDAJI WA TAKUKURU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/nacsap-iii-imeongea-mageuzi-ya-utendaji.html
0 Response to "NACSAP III IMEONGEA MAGEUZI YA UTENDAJI WA TAKUKURU"
Post a Comment