Loading...

NDITIYE AMFUKUZA MSIMAMIZI WA UJENZI WA BANDARI YA NYEMIREMBE,WILAYANI CHATO.

Loading...
NDITIYE AMFUKUZA MSIMAMIZI WA UJENZI WA BANDARI YA NYEMIREMBE,WILAYANI CHATO. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NDITIYE AMFUKUZA MSIMAMIZI WA UJENZI WA BANDARI YA NYEMIREMBE,WILAYANI CHATO., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NDITIYE AMFUKUZA MSIMAMIZI WA UJENZI WA BANDARI YA NYEMIREMBE,WILAYANI CHATO.
link : NDITIYE AMFUKUZA MSIMAMIZI WA UJENZI WA BANDARI YA NYEMIREMBE,WILAYANI CHATO.

soma pia


NDITIYE AMFUKUZA MSIMAMIZI WA UJENZI WA BANDARI YA NYEMIREMBE,WILAYANI CHATO.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amemfukuza msimamizi wa ujenzi wa bandari ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato mkoani Geita kwa kukosa sifa na utaalam wa kusimamia ujenzi wa bandari hiyo na miundombinu yake na kuagiza aondolewe mara moja kwenye eneo hilo

Hayo yamejitokeza wakati wa ziara ya Nditiye ya kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa bandari hiyo na miundombinu yake ambapo mkandarasi wa kampuni ya V.J Mistry & Co. Ltd amepewa jukumu hilo na Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ya kujenga bandari hiyo kwa gharama ya shilingi bilioni 4.128.

Katika ziara hiyo, Nditiye amebaini kuwa msimamizi wa ujenzi wa bandari hiyo Bwana Pravin Rabadhia wa mkandarasi wa kampuni ya V.J Mistry & Co. Ltd, hana utaalamu, sifa wala vigezo vyovyote vya kusimamia mradi huo unaogharimu matumizi ya fedha nyingi zinazotokana na fedha za makusanyo ya kodi ya wananchi. Pia, alibaini uwepo wa Bwana Dipak Chaganlal, mfanyakazi wa kampuni hiyo ya mkandarasi aliyejitambulisha kwa Nditiye kuwa ana taaluma ya “storekeeper” akiwa msimamizi msaidizi wa mradi wa ujenzi wa bandari hiyo.

Nditiye alielekeza msimamizi huyo aondolewe eneo la mradi wa ujenzi wa bandari ya Nyemirembe na mamlaka husika za vibali vya ajira, uhamiaji na mamlaka nyingine za manunuzi, bodi za makandarasi nchini zimchunguze taaluma yake, uraia wake, uhalali wake wa kufanya kazi ya kuwa msimamizi wa mradi huo kwa kuwa katika mahojiano nae akiwa kwenye eneo la mradi huo, wasimamizi hao wenye asilia ya kiasia hawakuweza kutoa maelezo yoyote ya kitaalamu kuhusu maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo.

Nditiye ameelekeza kuwa kazi hiyo ya ujenzi wa bandari ya Nyemirembe isimame kwa muda wa wiki moja na amemtaka mkandarasi wa kampuni hiyo kufika na kuripoti ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita mara moja akiwa na wataalamu wanaohitajika kufanya kazi hiyo kuendana na matakwa ya mkataba husika na kuhakikisha kuwa wafanyakazi na vibarua wote wanalipwa fedha zao .
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa bandari ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato, Geita. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akimhoji mfanyakazi wa mkandarasi wa kampuni ya V.J Mistry & Co. Ltd Bwana Dipak Chaganlal (mwenye asili ya kiasia) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa bandari ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato, Geita. Mwenye kofia nyeusi ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel
Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Bwana Morris Mtindichiusa akiandika maelekezo ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato, Geita. Mwenye kofia nyeusi ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel 
Wafanyakazi wa kampuni ya mkandarasi ya V.J Mistry & Co. Ltd wakiendelea na kazi mbali mbali za ujenzi wa bandari ya Nyemirembe iliyopo wilayani Chato, Geita wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi n Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo.




Hivyo makala NDITIYE AMFUKUZA MSIMAMIZI WA UJENZI WA BANDARI YA NYEMIREMBE,WILAYANI CHATO.

yaani makala yote NDITIYE AMFUKUZA MSIMAMIZI WA UJENZI WA BANDARI YA NYEMIREMBE,WILAYANI CHATO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NDITIYE AMFUKUZA MSIMAMIZI WA UJENZI WA BANDARI YA NYEMIREMBE,WILAYANI CHATO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/nditiye-amfukuza-msimamizi-wa-ujenzi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NDITIYE AMFUKUZA MSIMAMIZI WA UJENZI WA BANDARI YA NYEMIREMBE,WILAYANI CHATO."

Post a Comment

Loading...