Loading...
title : OCD Kyerwa ashushwa cheo,ahamisishwa
link : OCD Kyerwa ashushwa cheo,ahamisishwa
OCD Kyerwa ashushwa cheo,ahamisishwa
Timu ya Uchunguzi ya wasindikizaji wa Kahawa ya magendo yaundwa
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Nchini limetuma kikosi cha uchunguzi kufatilia tuhuma za askari waliokuwa wakisindika Kahawa ya Magendo wilayani Kyerwa mkoani Kagera.
Uchunguzi huo unatokana na kauli ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ya kutaka kufanyika uchunguzi kwa askari hao waliohusika kusindikiza Kahawa ya magendo.
Akizungumza na waandishi habari Jijini Dar es Salaam Msemaji wa Jeshi la Polisi Barnabas Mwakalukwa amesema katika uchunguzi huo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kyerwa (OCD) Justine Joseph ameshushwa cheo pamoja na kuhamishwa katika Kituo cha kazi.
Amesema aliyekuwa OCD wa Wilaya Kyerwa Justine Joseph amehamishiwa mkoani Iringa na kuwa chini ya uangalizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa.
Amesema uchunguzi huo ukikamilika watatoa majibu kwa wale waliohusika na tuhuma za usindikizaji wa Kahawa ya magendo.
Aidha amesema kuwa wakati Polisi wanafanya operesheni wananchi wanatakiwa kutii amri hiyo.
Mwakalukwa amesema tukio lilotokea mkoani Songwe la Mtu kupigwa risasi ilitokana na wananchi kutotii amri ya polisi wakati wakifanya operesheni ya waganga wa jadi lambalamba.
"Amri ya Polisi inatakiwa wananchi watii ili kuweza kuepuka na madhara yatayotokea mara baada ya kusaidia"amesema Mwakalukwa.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Barnabas Mwakalukwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Hivyo makala OCD Kyerwa ashushwa cheo,ahamisishwa
yaani makala yote OCD Kyerwa ashushwa cheo,ahamisishwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OCD Kyerwa ashushwa cheo,ahamisishwa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/ocd-kyerwa-ashushwa-cheoahamisishwa.html
0 Response to "OCD Kyerwa ashushwa cheo,ahamisishwa"
Post a Comment