Loading...

"PANGA" LA DC MJEMA LAFYEKA VISHOKA SOKO LA ILALA.

Loading...
"PANGA" LA DC MJEMA LAFYEKA VISHOKA SOKO LA ILALA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa "PANGA" LA DC MJEMA LAFYEKA VISHOKA SOKO LA ILALA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : "PANGA" LA DC MJEMA LAFYEKA VISHOKA SOKO LA ILALA.
link : "PANGA" LA DC MJEMA LAFYEKA VISHOKA SOKO LA ILALA.

soma pia


"PANGA" LA DC MJEMA LAFYEKA VISHOKA SOKO LA ILALA.


MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema,amewataka wale wote wanaojihusisha na Biashara ya kuwapangishia watu maeneo ya Serikali pembezoni Mwa barabara kuacha Mara moja.



Amesema kumezuka mchezo  wa watu wanaopangisha wafanya Biashara maeneo ya wazi ambayo hayapo katika utaratibu ambapo amesema kitendo hicho hata kivumilia katika Wilaya yake.
Hayo ameyasema akitembelea Soko la  Ilala boma katika ziara yake Kata ya Ilala  ili kujua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi na wafanya Biashara wa eneo hilo.

 Aidha , DC Mjema, ameitaka TAKUKURU, Manispaa ya Ilala kuhakikisha wanachukua hatua stahiki kwa kuwaweka ndani watakaohusika na utapeli huo.

 " Nani amewatuma mpangishe? Nataka kusema kwamba hicho kitendo mnachokifanya kitawapeleka motoni , eneo hili si lakwako ni la  Serikali Sasa wewe unavyo jibinafsisha unavunja Sheria, Afisa TAKUKURU nakuomba fuatilia hili na utoe majibu  wato watakao husika sweka ndani" Amesema DC Mjema.

 Katika hatua nyingine, DC Mjema, amewataka wafanya Biashara wote waliopo katika Soko hilo kujisajili ili waweze kutambulika kisheria na kuingizwa katika orodha ya wafanya Biashara waliopo katika Wilaya ya Ilala.

Amesema faida za kuingizwa katika usajili ni pamoja na kutambulika, kupata vitambulisho vya Taifa, kukopesheka katika Mabenki na kutanua wigo wa Biashara zao Kimataifa ndani na nje ya nchi.

 " Hatutaki kuona mfanya Biashara katika Wilaya yangu ananyanyasika , Rais wetu John Magufuli, amesema tusiwahamishe mpaka tupate maeneo ya kuwaweka, Sasa mkijiandikisha na kutambulika Habari ya kukimbizwa kimbizwa itakufa, maana yake tutakapoingia katika Soko Letu jipya kipaumbele cha kwanza mtapatiwa nyie kwanza na kubadilisha maisha yenu kuelekea katika uchumi wa Kati" Amesisitizia DC Mjema.

Pia amesema kwa Sasa   wamesharatibu masoko, ambapo kuna masoko matatu ya kisasa yatakayo jengwa, Miongoni Mwa Masoko hayo ni pamoja na Soko la Kisutu ambalo lipo katika hatua za ujenzi, Soko la  Karume pamoja na Soko la  Ilala Boma.

Amewataka wafanya Biashara kufanya kazi kwa uhuru na tozo ndogo ndogo zinazotozwa kinyume na Sheria atahakikisha zinafutwa zote kwa kuwa Serikali ya awamu ya tano ni ya Wanyonge na masikini.

 Amesema wale wote waliowapangisha wafanya Biashara wenzao wakati wa zoezi la  usajili maeneo hayo wapewe waliopangishwa ili wayamiliki kwa kuwa wao wapangishwaji ndio wanashida.

 Amewataka wananchi wa kata ya Ilala, waendelee kutoa ushirikiano dhidi ya Viongozi wao na pindi wanapoona mambo hayaendi sawa Ofisi yake ipo  wazi itawasikiliza na kuwajibu.

Mbali na DC Mjema, Diwani wa kata ya Ilala, Saady Khimji, amemshukuru mkuu wa Wilaya huyo kwa kuacha kazi zake na kwenda kuwatembelea jambo alilosema halijawahi kufanywa na mkuu wa Wilaya yoyote katika Wilaya hiyo.

Khimji, amesema wananchi wake ni wasikivu katika kuona kata yao inapata maendeleo pamoja na changamoto za hapa na pale.

Pia khimji, amesema Mtaa wa Kasongo  ni miongoni Mwa Mitaa iliyokuwa na shida ya Mafuriko wakati wa Mvua lakini kwa Sasa wamefanikiwa kujenga mfereji na hali ipo  shwari.

Diwani huyo, amesema kwamba, mfereji huo ulitumia Shilingi Milioni 11 ambapo Milioni 6 zilichangwa na nguvu ya Wananchi kwa kuchangisha kila mtu  Shilingi 150000 na Milioni 5 zilitoka katika mfuko wa Jimbo.

 Ikumbukwe kwamba, Kata ya Ilala ni kata mama katika Jiji la  Dar es Salaam, kata hiyo ina  jumla ya Mitaa 5, Sharifi Shamba, Karume, Kasongo, Mtaa wa kasuru pamoja na Mafuriko huku ukiwa na jumla ya Shule 4 ambapo Shule 2 za Serikali na 2 za watu binafsi na Shule za Msingi 10.

 Katika huduma za Afya, Kata hiyo ina  Taasisi moja ya Hospitali ya Amana  na zahanati za watu binafsi huku Viwanda vingi vikionekana kutokuwa na uwezo ambapo ni kiwanda kimoja tu cha TBL kinachotambulika.










Hivyo makala "PANGA" LA DC MJEMA LAFYEKA VISHOKA SOKO LA ILALA.

yaani makala yote "PANGA" LA DC MJEMA LAFYEKA VISHOKA SOKO LA ILALA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala "PANGA" LA DC MJEMA LAFYEKA VISHOKA SOKO LA ILALA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/panga-la-dc-mjema-lafyeka-vishoka-soko.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to ""PANGA" LA DC MJEMA LAFYEKA VISHOKA SOKO LA ILALA."

Post a Comment

Loading...