Loading...
title : RC MAKONDA APATIA UFUMBUZI KERO SUGU ZA WANANCHI WA BUGURUNI.
link : RC MAKONDA APATIA UFUMBUZI KERO SUGU ZA WANANCHI WA BUGURUNI.
RC MAKONDA APATIA UFUMBUZI KERO SUGU ZA WANANCHI WA BUGURUNI.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana amefanya ziara ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
RC Makonda amesema wananchi tunapaswa kuunga mkono juhudi za serikali za ujenzi wa Reli ya kisasa (standard gauge) ambayo inaenda kulifikisha taifa katika uchumi wa kati na kuitangaza Tanzania katika ramani ya Dunia hivyo amewasihi wananchi waliovunjiwa kuwa wavumilivu.
Aidha RC Makonda ameiomba kampuni hodhi ya rasilimali za reli RAHCO kuangalia uwezekano wa kuwapatia wananchi angalau njia za kupita ili kuwapunguzia mizunguko mirefu.Katika ziara hiyo RC Makonda amemuagia Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa kumuhamisha kituo kingine mkuu wa kituo cha Polisi Buguruni kwakuwa watu anaowaongoza hawamuamini.
Hata hivyo RC Makonda ametoa siku Saba kwa kigogo wa Bodi ya Mikopo kumkabidhi bajaji kijana alietambulika kwa jina la Jafari Raphael aliegongwa na gari na kigogo huyo na kupelekea ulemavu wa kukatwa mguu mmoja pasipo kulipwa fidia yoyote na kumfanya kijana huyo kugeuka kuwa mtu wa kuomba misaada huku kigogo huyo akiendelea kula maisha na familia yake.
Pamoja na hayo RC Makonda amepatia ufumbuzi kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili Umoja wa Madereva wa daladala buguruni Chama waliokuwa wamezuiwa kuegesha magari eneo la Buguruni station ambapo RC Makonda amewaagiza madereva hao kurudi katika eneo hilo.
Miongoni mwa kero zilizotolewa na wakazi wa buguruni ni pamoja na tozo kubwa ya uchafu, polisi jamii,ukamataji wa watu, watu kubambikiziwa kesi, migogoro ya mirathi na watu kudhulumiwa ambapo RC Makonda amezipatia majibu kero hizo papo kwa papo kwa kupigia simu kwa walengwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na Wakazi wa eneo la Buguruni jana,alipofanya ziara ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa eneo hilo ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akisikiliza moja ya swali kutoka kwa mkazi wa Buguruni jana,wakati Makonda alipofanya ziara ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na ujumbe wake alipokuwa akiwasili maeneo ya Buguruni jana,katika ziara yake ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na mmoja wakazi wa Buguruni ,katika ziara yake ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
Hivyo makala RC MAKONDA APATIA UFUMBUZI KERO SUGU ZA WANANCHI WA BUGURUNI.
yaani makala yote RC MAKONDA APATIA UFUMBUZI KERO SUGU ZA WANANCHI WA BUGURUNI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA APATIA UFUMBUZI KERO SUGU ZA WANANCHI WA BUGURUNI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/rc-makonda-apatia-ufumbuzi-kero-sugu-za.html
0 Response to "RC MAKONDA APATIA UFUMBUZI KERO SUGU ZA WANANCHI WA BUGURUNI."
Post a Comment