Loading...

SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO

Loading...
SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO
link : SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO

soma pia


SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO

Na Greyson Mwase, Sumbawanga

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini ipo tayari kuwasaidia wawekezaji kwenye shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini ili uchimbaji wao ulete manufaa kwa nchi.

Aliyasema hayo leo tarehe 12 Oktoba, 2018 mara baada ya kumaliza ziara yake katika mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited uliopo katika kijiji cha Nkomolo II Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Katibu Tawala Msaidizi – Sehemu ya Miundombinu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Happiness Shayo, Wataalam wa Madini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na waandishi wa habari.

Alisema kuwa katika kuhakikisha watafiti na wachimbaji wa madini wanafanya kazi katika mazingira mazuri, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeanza kusogeza huduma zake kwa kuhakikisha kuwa inaanzisha ofisi za maafisa madini wakazi katika mikoa yote ambapo mkoa wa Rukwa unatarajiwa kupata ofisi kwa mara ya kwanza.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo aliushauri uongozi wa mgodi huo kujikita kwenye uzalishaji wa makaa ya mawe ambayo ni bora na kuuza katika nchi za jirani kwa kuwa mahitaji ya makaa ya mawe ni makubwa.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ( wa kwanza mbele) akiendelea na ziara katika mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited uliopo katika kijiji cha Nkomolo II Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa. 
Meneja wa mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited, Jamhuri Mbamba (kushoto) akimwonesha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) moja ya makaa ya mawe kwenye mgodi huo. 
Meneja wa mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited, Jamhuri Mbamba (katikati) akielezea hali ya uzalishaji wa makaa ya mawe katika mgodi huo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) katika ziara hiyo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>


Hivyo makala SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO

yaani makala yote SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/serikali-ipo-tayari-kusaidia-wawekezaji.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI IPO TAYARI KUSAIDIA WAWEKEZAJI WA MADINI-NYONGO"

Post a Comment

Loading...