Loading...

SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA

Loading...
SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA
link : SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA

soma pia


SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA

*Asema zaidi ya wakulima wadogo 527,000 katika Mikoa 13 wamenufaika 

WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 56.45 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kilimo katika mikoa 13 hapa nchini.

Amesema mikopo hiyo imetolewa katika kipindi cha kuanzia Agosti 2015 hadi  Septemba 2018, kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 3, 2018) kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) mjini Mororogo.

Mikopo hiyo imewanufaisha wakulima wadogo zaidi ya 527,000 waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya kahawa, karafuu, mahindi, mbogamboga na mazao mengine.Amesema Serikali inatekeleza mipango mbalimbali kwa lengo la kutatua kero zinazowakabili na kuwawezesha wakulima wadogo kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo. 

Amesema Juni 14, mwaka huu Rais Dkt. John Magufuli, alizindua Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo hapa nchini (ASDP II) yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo.Waziri Mkuu amesema ASDP II inalenga kuhakikisha sekta ya kilimo inapewa kipaumbele stahiki ili iweze kuleta tija kwa wakulima wenyewe na Taifa kwa ujumla.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo kutoa mikopo kwa wakulima wadogo; kuondoa baadhi ya tozo zenye kufifisha uzalishaji.” Pia kuweka mipango mizuri ya matumizi bora ya ardhi na kutafuta masoko pamoja na kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo ili kumuongezea tija mkulima.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018.
Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uswiss nchini, Florence Tinguely Mattli katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro, Octoba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa uyoga, Maria Shindika wa Mvomero (kulia) kabla ya kuhutubia katika Maadhidhimisho ya Miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (MVIWATA) yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Oktoba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu unga na bidhaa mbalimbali zinaotokana na zao la soya kutoka kwa Julie Bwire wa Mvomero (kushoto) kabla ya kuhutubia katika Maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Oktoba 3, 2018. 





Hivyo makala SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA

yaani makala yote SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/serikali-yawapa-wakulima-mikopo-ya-sh.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YAWAPA WAKULIMA MIKOPO YA SH. BIL. 56.45-MAJALIWA"

Post a Comment

Loading...