Loading...

SITAMVUMILIA ANAYEIHUJUMU NHIF- RC MBEYA

Loading...
SITAMVUMILIA ANAYEIHUJUMU NHIF- RC MBEYA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SITAMVUMILIA ANAYEIHUJUMU NHIF- RC MBEYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SITAMVUMILIA ANAYEIHUJUMU NHIF- RC MBEYA
link : SITAMVUMILIA ANAYEIHUJUMU NHIF- RC MBEYA

soma pia


SITAMVUMILIA ANAYEIHUJUMU NHIF- RC MBEYA

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
SERIKALI mkoani Mbeya imesema itachukua hatua kali kwa mtu yeyote atakayejihusisha na udanganyifu wa huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Onyo hilo  limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Albert Chalamila wakati akifungua mkutano wa wadau wa NHIF mkoani humo. “Kufanya udanganyifu kwa huduma za Mfuko ni kuhujumu jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali za kumairisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi, hivyo ndani ya Mkoa huu sitavumilia kuona hili.
 “Tunasikia kuna baadhi ya wadau wa Mfuko wasio waaminifu wamekuwa wakihujumu Mfuko huu, kwa upande wa Mkoa wa Mbeya niliweke tu wazi kuwa atakayejihusisha na udanganyifu wowote nitakula naye sahani moja, ni lazima huu Mfuko tuulinde ili uweze kuhudumia wananchi na hata vizazi vijavyo,” alisema Bw. Chalamila.
Ili kuhakikisha huduma za Mfuko zinalindwa, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wadau wote mkoani humo kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Akisisitiza juu ya wananchi kujiunga na huduma za Mfuko, ameweka wazi kuwa ili taifa liweze kufikia malengo yake na kutimiza ndoto ya Rais Dkt. John Magufuli ya Tanzania kuwa ni nchi ya Uchumi wa Kati kupitia uwekezaji wa Viwanda ni lazima huduma za matibabu ziwe za uhakika kwa wananchi wote.
“Ni azma ya Serikali hii kuwafikia watanzania wote na huduma bora za matibabu kupitia Bima ya Afya, kukamilika kwa azma hii kutaruhusu watu wengi zaidi kutumia huduma za matibabu ambazo awali walishindwa hivyo niwaombe tu watoa huduma mjipange kuweka mazingira mazuri ya kuwahudumia watu hawa,” alisema Mkuu wa Mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Albert Chalamila akifungua mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani humo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda akihutubia wadau wa mkutano huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Beranrd Konga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mfuko kwa Wadau wa Mkoa wa Mbeya.

 Sehemu ya Wajumbe wa Bodi ya NHIF wakifuatilia taarifa ya utekelezaji.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala SITAMVUMILIA ANAYEIHUJUMU NHIF- RC MBEYA

yaani makala yote SITAMVUMILIA ANAYEIHUJUMU NHIF- RC MBEYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SITAMVUMILIA ANAYEIHUJUMU NHIF- RC MBEYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/sitamvumilia-anayeihujumu-nhif-rc-mbeya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SITAMVUMILIA ANAYEIHUJUMU NHIF- RC MBEYA"

Post a Comment

Loading...