Loading...

TFDA, TBS, GCLA, TAFFA WAKUTANA KUTATUA KERO KATIKA UTENDAJI WAO.

Loading...
TFDA, TBS, GCLA, TAFFA WAKUTANA KUTATUA KERO KATIKA UTENDAJI WAO. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TFDA, TBS, GCLA, TAFFA WAKUTANA KUTATUA KERO KATIKA UTENDAJI WAO., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TFDA, TBS, GCLA, TAFFA WAKUTANA KUTATUA KERO KATIKA UTENDAJI WAO.
link : TFDA, TBS, GCLA, TAFFA WAKUTANA KUTATUA KERO KATIKA UTENDAJI WAO.

soma pia


TFDA, TBS, GCLA, TAFFA WAKUTANA KUTATUA KERO KATIKA UTENDAJI WAO.

 Wadau mbalimbali wakiwa katika Mkutano leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
 Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya mkemia mkuuu wa Serikali Dkt. Fidelince Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imewataka wadau mbalimbali hapa nchini kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha wanaleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.

Wadau hao ni Shirika la Viwango (TBS), Mawakala ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) pamoja na  Chama cha Mawakala wa forodha Tanzania (TAFFA) ambao wamekutana leo kwa ajili ya kujadili taratibu za uingizaji wa bidhaa hapa nchini 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Agnes Kijo, amesema kuwa mkutano umelenga kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utendaji.

Agnes amesema kuwa mkutano ni muhimu kutokana kila mdau amepata fursa ya kueleza majukumu yake katika utendaji pamoja na kuangalia matakwa ya kisheria ambayo imekuwa ikitumika.

"Uwepo wa mkutano huu kwetu TFDA ni jambo jema kutokana majukumu yetu ni kuaangalia usalama wa chakula kutokana na bidhaa zinazoingizwa hapa nchini" amesema Agnes.

Amesema kuwa ni vizuri kuaangalia kila jambo liwe linakwenda vyema katika kufanikisha maendeleo katika kuzuia bidhaa feki ambazo zimekuwa zikiingia hapa nchini kinyume na sheria.

Agnes amefafanua kuwa taasisi zote ambazo zimeshiriki mkutano huo zina nia ya kujirekebisha ili kuhakikisha kila mmoja nafanya kazi yake kikamilifu.

"Kumekuwa sitofahamu utaratibu wa kuingiza bidhaa kwani watu wa forodha wamekuwa wakichelewa kutoa mizigo kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kuchelewa kuomba kwa vibali" amesema Agnes.

Hata hivyo ameeleza kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kukusanya kero za wadau mbalimbali na kuzifanyia kazi jambo ambalo linaweza kuleta ufanisi katika utendaji.

Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya mkemia mkuuu wa Serikali Dkt. Fidelince Mafumiko, amesema kuwa mkutano huo utawapa fursa ya kupata mrejesho katika huduma wanazotoa taasisi mbalimbali.

Dkt. Mafumiko amesema kuwa ni mwanzo mkubwa mzuri katika kutengeneza mipango ya kuendelea kutoa huduma bora.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango (TBS) Lazaro Msasalaga, amesema kuwa mkutano utasaidia kuongeza ufanisi katika mpango wa utoaji wa mizigo kwa kutatua changamoto zinazotukabili katika taasisi.

"Tumekutana na Mawakala wa forodha katika kuangalia changamoto ambazo zipo ili zifanyiwe kazi" amesema Msasalaga.



Hivyo makala TFDA, TBS, GCLA, TAFFA WAKUTANA KUTATUA KERO KATIKA UTENDAJI WAO.

yaani makala yote TFDA, TBS, GCLA, TAFFA WAKUTANA KUTATUA KERO KATIKA UTENDAJI WAO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TFDA, TBS, GCLA, TAFFA WAKUTANA KUTATUA KERO KATIKA UTENDAJI WAO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/tfda-tbs-gcla-taffa-wakutana-kutatua.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TFDA, TBS, GCLA, TAFFA WAKUTANA KUTATUA KERO KATIKA UTENDAJI WAO."

Post a Comment

Loading...