Loading...
title : THE DESK &CHAIR YATOA VIFAA TIBA VYA WALEMAVU WA MACHO
link : THE DESK &CHAIR YATOA VIFAA TIBA VYA WALEMAVU WA MACHO
THE DESK &CHAIR YATOA VIFAA TIBA VYA WALEMAVU WA MACHO
Na Baltazar Mashaka, Mwanza
SERIKALI mkoani Mwanza imepokea msaada wa vifaa tiba na upasuaji kwa walemavu wa macho vilivyotolewa na The Desk & Chair Foundation (TD & CF) Tawi la Tanzania.
Vifaa hivyo vitakavyotumika kwenye kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Fimbo Nyeupe yanayofanyika kitaifa jijini humu, vilipokelewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa The Desk & Cir Foundation Sibtain Meghjee alisema wanaunga mkono juhudi za serikali za kuhudumia jamii kwa kuwa taasisi hiyo inatambua watu wenye ulemavu wana changamoto nyingi zikiwemo kushindwa kumudu gharama za matibabu.
“Taasisi hii inafanya shughuli za kusaidia jamii (walemavu,wagonjwa na masuala ya elimu),kulingana na mahitaji.Kwa changamoto za walemavu wa macho ni kushindwa kumudu gharama za tiba sababu ya ugumu wa kipato hivyo serikali iangalie jinsi ya kuwasidia wapate Bima ya Afya,”alisema Meghjee.
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo Mongela alisema maadhimisho ya ya Fimbo Nyeupe ni kielelezo kuwa walemavu wana mchango mkubwa na ndiyo maana TEHAMA inawaelekeza kwenye Uchumi wa Viwanda kama ilivyo kauli mbiu.
Alisema vifaa hivyo vitahudumia wilaya saba za Mkoa wa Mwanza na hivyo serikali imejipanga wananchi watakaojitokeza hawatakosa huduma kwenye maadhimisho hayo na kambi ya uchunguzi wa macho, watakaobainika watatibiwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure.
Mwenyekiti wa The Desk Chair Foundation Sibatain Meghjee akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba vya macho na upasuaji kwa serikali ya Mkoa wa Mwanza. Kushoto wa kwanza ni Katibu Tawala Msaidizi Seif Rashid, wa pili ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagan Dk. Philis Nyimbi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Silas Wambura akizungumza kuhusu ubora wa vifaa hivyo kabla ya kukabidhiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi,akipokea vifaa tiba na upasuaji pamoja na fimbo nyeupe kutoka kwa Mwenyekiti wa Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizungumza baada ya kupokea msaada wa fimbo nyeupe, vifaa tiba vya macho na upasuaji vilivyotolewa an The Desk & Chair Foundation.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala THE DESK &CHAIR YATOA VIFAA TIBA VYA WALEMAVU WA MACHO
yaani makala yote THE DESK &CHAIR YATOA VIFAA TIBA VYA WALEMAVU WA MACHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala THE DESK &CHAIR YATOA VIFAA TIBA VYA WALEMAVU WA MACHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/the-desk-yatoa-vifaa-tiba-vya-walemavu.html
0 Response to "THE DESK &CHAIR YATOA VIFAA TIBA VYA WALEMAVU WA MACHO"
Post a Comment