Loading...

Ujerumani ‘kumenoga’ waipiga jeki Sauti za Busara 2019

Loading...
Ujerumani ‘kumenoga’ waipiga jeki Sauti za Busara 2019 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ujerumani ‘kumenoga’ waipiga jeki Sauti za Busara 2019, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ujerumani ‘kumenoga’ waipiga jeki Sauti za Busara 2019
link : Ujerumani ‘kumenoga’ waipiga jeki Sauti za Busara 2019

soma pia


Ujerumani ‘kumenoga’ waipiga jeki Sauti za Busara 2019

Na Andrew Chale. Dar es Salaam.
Serikali ya Ujerumani kupitia kwa Balozi wake Nchini Tanzania, Dkt. Detlef  Waechter imetiliana saini ya ufadhili na Taasisi ya Busara Promotions waandaaji wa tamasha la Sauti za Busara linalofanyika kila mwaka visiwani Zanzibar.
Ujerumani imekubali kuchangia fedha ambazo zitaenda kufanikisha shughuli za tamasha hilo msimu wa 16, mwakani 2019.
Hafla hiyo imefanyika Oktoba 18, 2018  katika ofisi za Ubalozi huo Jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo la kutiliana saini, limewahusisha Balozi huyo wa Ujerumani nchini Dkt. Detlef  Waechter  pamoja na Mwenyekiti wa Tamasha hilo la Sauti za Busara, Mheshimiwa Simai Mohammed Said ambaye pia (Mwakilishi jimbo la Tunguu).
Ufadhili huo ni juhudi za Wizara ya Mambo ya Nje ya nchini Ujerumani  katika kuunga mkono utamaduni wa Tanzania kwa kufadhili Tamasha hilo la kimataifa la Muziki ambalo limekuwa pia kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi visiwani Zanzibar.
Balozi Dkt. Detlef Waechter amemwakikishia  Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza utamaduni wa Mtanzania kwa kuongeza fursa na tija zitokanazo na zao la ushirikiano wa Nchi hizo mbili.
Kwa upande wao Busara Promotions wamesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo lenye kauli mbiu “Where African Music Stars Shine Brightly”, yanaendelea na tayari wamechapisha majina ya Wasanii na bendi pamoja na Nchi wanazotoka miongoni mwao ni Staa wa muziki wa Hip Hop Fareed Kubanda maarufu kama “Fid Q” kutoka Tanzania.
Pia wapo: Mokoomba (Zimbabwe), Afrigo Band (Uganda), Fadhilee Itulya (Kenya), Ifrikya Spirit (Algeria), Rajab Suleiman & Kithara ( Zanzibar), Tune Recreation Committee, (Afrika Kusini), Ithrene (Algeria).
Wengine ni: Hoba Hoba Spirit (Morocco), M'Toro Chamou (Mayotte/Reunion), Trio Kazanchis +2 (Ethiopia/Switzerland), Faith Mussa (Malawi), Shamsi Music (Kenya), Sofaz  (Reunion), Dago Roots( Reunion), Lydol  (Cameroun), Jackie Akello (Uganda).
Wamo pia: S Kide & Wakupeti Band (Tanzania), Tausi Women's Taarab (Zanzibar), Mkubwa na Wanawe Crew (Tanzania), Damian Soul (Tanzania) na  Wamwiduka Band (Tanzania).
Tamasha  hilo la 16 litafanyika Mji Mkongwe Zanzibar kuanzia tarehe 7 – 10 February 2019 huku  majukuwaa 3 tofauti yatawaka moto kwa muziki wa moja kwa moja ‘live’ kwa muda wa siku zote za tamasha kuanzia asubuhi, mchana na Usiku.
Na Andrew Chale


Hivyo makala Ujerumani ‘kumenoga’ waipiga jeki Sauti za Busara 2019

yaani makala yote Ujerumani ‘kumenoga’ waipiga jeki Sauti za Busara 2019 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ujerumani ‘kumenoga’ waipiga jeki Sauti za Busara 2019 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/ujerumani-kumenoga-waipiga-jeki-sauti.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Ujerumani ‘kumenoga’ waipiga jeki Sauti za Busara 2019"

Post a Comment

Loading...