Loading...
title : UKOSEFU WA UWAJIBIKAJI NA UWAZI CHANZO CHA MIGOGORO AZAKI
link : UKOSEFU WA UWAJIBIKAJI NA UWAZI CHANZO CHA MIGOGORO AZAKI
UKOSEFU WA UWAJIBIKAJI NA UWAZI CHANZO CHA MIGOGORO AZAKI
Ukosefu wa uwazi na uwajibikaji katika shughuli za Asasi za Kiraia Tanzania unaathiri uwezo wa nchi kutambua kiwango cha michango na misaada inayotolewa na wadau wa maendeleo na matokeo yake katika maendeleo ya nchi.
Hayo yamesema jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Wa Asasi za KIrai Tanzania katika hotuba aliyoitoa kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kasimu Majaliwa wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Asasi za Kirai Tanzania.
Dkt. Jingu aliongeza kuwa ukosefu wa uwazi na uwajibikaji wa baadhi ya AZAKI unatoa fursa ya rasilimali za umma ambazo hutolewa kwao kutumika vibaya na hivyo kuathiri kufikiwa kwa matokeo yanayotarajiwa.
Katibu Mkuu huyo aliendelea kusema kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha malalamiko na manung’uniko kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafadhili wao na walengwa wa miradi yao.
“Ukosefu wa uwazi umekuwa chanzo cha migogoro miongoni mwa wanachama wa AZAKI husika. Pia, kukosekana kwa uwazi na uwajibikaji kumesababisha baadhi ya AZAKI kutumika vibaya kinyume na sheria za nchi na kinyume malengo ya kuanzishwa kwao’’. Aliongeza Dkt Jingu.
Pamoja na mapungufu hayo Dkt. Jingu amezisifu Asasi hizo za Kiraia kuwa zinatoa mchango mkubwa katika kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma na kuleta uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa mali za umma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,Dkt John Jingu akikata utepe kufungua maonesho ya Wiki ya Asasi za Kiraia Tanzania AZAKI yanayofanyika jijini Dodoma kwa siku tano kuanzia Oktoba 22-26, 2018.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,Dkt John Jingu akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia Tanzania AZAKI inayoendelea leo jijini Dodoma Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu Profesa Faustine Kamuzora na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usajili na Uratibu Wa NGOs Bw. Leornard Baraka .
Kaimu Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,Bw. Leornad Baraka akijibu hoja za wadau Wiki ya Asasi za Kiraia Tanzania AZAKI yanayofanyika jijini Dodoma kwa siku tano kuanzia Oktoba 22-26, 2018 kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,Dkt John Jingu.
Baadhi ya wadau wa Mkutano wa Asasi za kiraia wakifuatilia kwa makini yanayojili katika Mkutano Mkuu wa Asasi za Kiraia Tanzania AZAKI unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tano kuanzia Oktoba 22-26, 2018. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala UKOSEFU WA UWAJIBIKAJI NA UWAZI CHANZO CHA MIGOGORO AZAKI
yaani makala yote UKOSEFU WA UWAJIBIKAJI NA UWAZI CHANZO CHA MIGOGORO AZAKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UKOSEFU WA UWAJIBIKAJI NA UWAZI CHANZO CHA MIGOGORO AZAKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/ukosefu-wa-uwajibikaji-na-uwazi-chanzo.html
0 Response to "UKOSEFU WA UWAJIBIKAJI NA UWAZI CHANZO CHA MIGOGORO AZAKI"
Post a Comment