Loading...
title : WADAU WANAUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUONGEZA UELEWA WA UWEKEZAJI KUPITIA MASOKO YA MITAJI-DKT MPANGO
link : WADAU WANAUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUONGEZA UELEWA WA UWEKEZAJI KUPITIA MASOKO YA MITAJI-DKT MPANGO
WADAU WANAUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUONGEZA UELEWA WA UWEKEZAJI KUPITIA MASOKO YA MITAJI-DKT MPANGO
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango amesema wadau wamekuwa na mwamko katika sekta ya fedha ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kisera kwa lengo la kuongeza uwelewa na kukuza uwekezaji kupitia masoko ya mitaji.
Mpango ameyasema hayo wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa shindano kuhusu Masoko na Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu pamoja na kutunuku vyeti kwa wahitimu wa kozi ya watendaji katika masoko ya Mitaji wanaokidhi viwango vya kimataifa iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa masoko na mitaji kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha hususani masoko ya mitaji na uchumi kwa ujumla hapa nchini.
Dkt. Mpango ameiagiza Mamlaka yay a Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuendelea kuandaa shindano hilo katika kuwajengea vijana wa kitanzania kujiamini na kuweza kuwa wabobezi katika eneo hilo.
Amesema shindano hilo kushirikisha wanafunzi zaidi ya 15000 sio kazi ndogo lakini ina manufaa kwa vijana wa kitanzania.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Masoko na Dhamana Nicodemus Mkama amesema kuwa washindi 12 kwa uwiano wa wasichana sita na wavulana sita waliopata alama za juu wamepata fedha sh.milioni 1.8 kwa kila mmoja na kupata safari mafunzo nchini Mauritius kujifunza mamlaka ya usimamizi wa Masoko ya Motaji ya nchi hiyo, Soko la Hisa Mauritius na kampuni tano kubwa za utoaji wa huduma katika masoko ya mitaji.
Mkama amesema CMSA inaendelea kufanya jitihada za kuongeza idadi wataalam wa masoko na mitaji yenye lengo la kuanzisha na kuendeleza masoko ya mitaji , yenye ufanisi , uwazi na yenye kutoa haki sawa kwa washiriki wote.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango akitoa zawadi kwa washindi wa shindano.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Masoko na Dhamana Nicodemus Mkama akitoa maelezo ya shindano hilo lililoratibiwa na Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuwapata vijana mahiri wa masoko ya mitaji katika hafla ya utoaji zawadi uliofanyika jijini Dar es es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa wanafunzi katika shiondano.
Hivyo makala WADAU WANAUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUONGEZA UELEWA WA UWEKEZAJI KUPITIA MASOKO YA MITAJI-DKT MPANGO
yaani makala yote WADAU WANAUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUONGEZA UELEWA WA UWEKEZAJI KUPITIA MASOKO YA MITAJI-DKT MPANGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WADAU WANAUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUONGEZA UELEWA WA UWEKEZAJI KUPITIA MASOKO YA MITAJI-DKT MPANGO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wadau-wanaunga-mkono-serikali-katika.html
0 Response to "WADAU WANAUNGA MKONO SERIKALI KATIKA KUONGEZA UELEWA WA UWEKEZAJI KUPITIA MASOKO YA MITAJI-DKT MPANGO"
Post a Comment