Loading...
title : Wadau wataka Kiswahili kitumike kama Lugha ya Kufundishia
link : Wadau wataka Kiswahili kitumike kama Lugha ya Kufundishia
Wadau wataka Kiswahili kitumike kama Lugha ya Kufundishia
Na Shamimu Nyaki – WHUSM
Wadau mbalimbali wameishauri Serikali kufikiria namna ya kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia shuleni ili kukuza na kuendeleza lugha hiyo ambayo ndio utambulisho wa Taifa letu.
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dodoma katika Mdahalo wa Kumbukizi ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K.Nyerere uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha ST.Jonhs of Tanzania ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadilia na washiriki.
Awali Mhe.Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Mwakyembe akifungua mdahalo huo alisema kuwa lugha ya Kiswahili ndio lugha kuu ya mawasiliano hapa nchini na ndio lugha inayowatambulisha watanzania Ulimwenguni. “Kiswahili hivi sasa ni lugha kubwa sana duniani na inazungumzwa na watu wengi hivyo ni lazima watanzania wakawa mstari wa mbele kukikuza na kukiendeleza kwa kukizungumza kwa ufasaha”.Alisema Dkt Mwakyembe.
Aidha Dkt. Mwakyembe amemuagiza Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw.Godfrey Muingereza kuhakikisha kuwa katika mashindano yajayo ya ulimbwende washiriki wanatumia lugha ya Kiswahili katika mashindano ya ndani na watakapoiwakilisha nchi kimataifa.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Susan Mlawi ameongeza kuwa mdahalo huo ni muendelezo wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa inayotarajiwa kufikia kilele chake Disemba 08 mwaka huu ambapo itatanguliwa na matukio tofauti kiwemo Mijadala,makongamano na nyimbo mbalimbali na kauli mbiu mwaka huu ni “Kiswahili Uhai wetu,Utashi wetu.”

.Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Mwakyembe .
Hivyo makala Wadau wataka Kiswahili kitumike kama Lugha ya Kufundishia
yaani makala yote Wadau wataka Kiswahili kitumike kama Lugha ya Kufundishia Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wadau wataka Kiswahili kitumike kama Lugha ya Kufundishia mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wadau-wataka-kiswahili-kitumike-kama.html
0 Response to "Wadau wataka Kiswahili kitumike kama Lugha ya Kufundishia"
Post a Comment