Loading...
title : WAJASIRIAMALI WAWEZESHWA KIUCHUMI
link : WAJASIRIAMALI WAWEZESHWA KIUCHUMI
WAJASIRIAMALI WAWEZESHWA KIUCHUMI
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa jimbo la Mkuranga abdallah Ulega ametoa sh.milioni mbili m kwa vikundi vya ujasiriamali 11 vya kata ya Kimanzimchana wilayani Mkuranga mkoani Pwani ikiwa ni lengo la kukuza mitaji yao na kuwainua kiuchumi wajasiriamali hao.
Akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo, Katibu wa Mbunge wa jimbo la Mkuranga Kisatu Omary amevitaja baadhi ya vikundi vilivyopewa fedha hizo kuwa ni Tupendane Group,Mshikmano pamoja na mazingira group.
Aidha Kisatu amesema ulega ametoa fedha hizo kwa lengo la kuinua mitaji yao, na kuwaomba kuzitumia kwenye malengo yaliyokusudiwa.
"Serikali inawapenda wananchi wake na ipotayari kuwasaidia mkiwa kwenye vikundi hivyo kwahiyo dumisheni vikundi vyenu mpate kukopesheka.
"Serikali inatoa fedha kwa ajili ya wajisiriamali ambayo ni asilimia kumi kupitia Halmashauri lakini ni lazima muwe kwenye vikundi tena vyenye sifa"amesema Kisatu.
Aidha Kisatu ameomba wajasiriamali hao kutumia hela hiyo kwa kukuza mitaji yao na sio kwenda kwa matumizi yao binafsi ili iweze kuleta tija na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga, Mariam Ulega akinunu miti kwa wajasiriamali wa kata ya Kimanzi chana Wilaya Mkuranga mkoa wa Pwani, ambapo kila kikundi kilipokea shilingi laki mbili kwajili ya kukuza mitaji yao.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Katibu wa Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Kisatu Omary akikabidhi zaidi ya sh.milioni mbili kwa vikudi vya wajasiriamali 11 vya kata ya Kimanzi chana Wilaya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Picha ya pamoja.
Hivyo makala WAJASIRIAMALI WAWEZESHWA KIUCHUMI
yaani makala yote WAJASIRIAMALI WAWEZESHWA KIUCHUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAJASIRIAMALI WAWEZESHWA KIUCHUMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wajasiriamali-wawezeshwa-kiuchumi.html
0 Response to "WAJASIRIAMALI WAWEZESHWA KIUCHUMI"
Post a Comment