Loading...
title : WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WAASWA KUJINOA NA MTOHANI YA BODI YA NBAA
link : WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WAASWA KUJINOA NA MTOHANI YA BODI YA NBAA
WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WAASWA KUJINOA NA MTOHANI YA BODI YA NBAA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam katika kozi ya uhasibu wameaswa kujinoa vizuri katika mitihani ya Bodi ya Uhasibu Nchini (NBAA) ili waweze kufanya vizuri katika mitihani hiyo ambayo itaanza hivi karibuni.
Akizungumza na wanafunzi wa wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam Afisa Mitihani wa Bodi ya Uhasibu (NBAA) Humphre Sympholian amesema kuwa mitihani ya bodi sio migumu kinachotakiwa kwa wanafunzi kujiandaa vizuri ambapo wanaweza kufanya vizuri.
Amesema kuwa kwa wale wanaofanya kazi katika kipindi kilichobaki waweze kuomba ruhusa ya kwa ajili ya kujiandaa na mitihani hiyo na kuweza kupata cheti mahususi kwa ajili ya uhasibu (CPA).Sympholian amesema kuwa mitihani hiyo wamekuwa mtihani wa bodi hiyo hauna upendeleo hivyo kila mtu atapata alichokipanda katika kujiandaa kwake na huo mtihani.
“Hatuna upendeleo kwani wanaosimamia sio ndio wanaosahihisha na kusahihisha huko hakuna majina ya wanafunzi kilichopo ni namba tu ambapo hawezi kupenya mwanafunzi wa kwa upendeleo”amesema Sympholian. Mhasibu na Mwalimu wa Chuo Kikuu Mzumbe Victirius Kamuntu amesema kuwa wanafunzi wake wamejiandaa na kuwa na imani kuwa mitihani ya bodi watatafanya vizuri.
Amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe katika mitihani ya bodi hiyo kwa wanafunzi chuo hicho wamekuwa wakifanya vizuri hivyo kukutana na watu wa bodi kunawafanya kuongeza juhudi ya kufikia malengo
Mwisho
Afisa Mitihani wa Bodi ya Uhasibu (NBAA) Humphre Sympholian akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuhusiana na mitihani ya Bodi itayofanyika hivi karibuni alipokutana na wanafunzi hao katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Afisa Mitihani wa NBAA, Rebecca Siame akieleza sheria zinazotumika na Bodi ya NBAA katika usimamizi wa Mitihani na mwanafunzi atakayebainika kufanya udanganyifu matokeo yake kufutwa wakati alipokutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wanaojiandaa na Mitihani ya Bodi ya Uhasibu Nchini(NBAA).
Hivyo makala WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WAASWA KUJINOA NA MTOHANI YA BODI YA NBAA
yaani makala yote WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WAASWA KUJINOA NA MTOHANI YA BODI YA NBAA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WAASWA KUJINOA NA MTOHANI YA BODI YA NBAA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wanafunzi-wa-chuo-kikuu-mzumbe-waaswa.html
0 Response to "WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE WAASWA KUJINOA NA MTOHANI YA BODI YA NBAA"
Post a Comment