Loading...

WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA

Loading...
WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA
link : WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA

soma pia


WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA

*Aweka hadharani idadi ya walipatikana wakiwa hai,na waliofariki dunia

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WATOTO 18 kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi mwaka huu wa 2018 wametekwa na kati yao 15 walipatilana wakiwa hai.Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola wakati anazungumza na waandishi wa habari.

Lugola amesema matukio ya kuteka watoto ambayo yameripotiwa katika kipindi cha mwaka 2016 hadi mwaka huu ni watoto 18, miongoni mwao walikuwa wa kiume sita na wa kike 12.

"Watoto 15 walipatikana wakiwa hai ,watoto wawili walipatikana wakiwa wamefariki na mtoto mmoja bado hajapatikana.Niwakumbushe wananchi kutoa taarifa za uhalifu wa utekaji mara tukio linapotokea ili Jeshi la Polisi lichukue hatua stahiki kwa wakati na kunusuru uhai wa wahusika," amesema Waziri Lugola.

UTEKWAJI WATU WAZIMA NDANI YA MIAKA MITATU

Wakati huo huo amesema juhudi za Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini zimefanikisha kuwapata watu watano wakiwa hai kati ya watu tisa waliokuwa wametekwa mwaka 2016.Amesema watu wanne hakupatikana na katika kipindi hicho watuhumiwa sita walikamatwa na watu watano walifikishwa mahakamani na mmoja aliuawa na wananchi.

Pia amesema mwaka 2017 walitekwa watu 27 ambapo Polisi walifanikiwa kuwapata watu 22 wakiwa hai na watu wawili walipatikana wakiwa wamekufa na watu watatu hawajapatikana.Watuhumiwa 11 walifikishwa mahakamani na watatu walifariki.

Waziri Lugola amesema katika kipindi cha Oktoba 11 mwaka 2018 watu 21 walitekwa ambapo kati yao 17 walipatikana wakiwa hai na wanne hawajapatikana hadi sasa.Watuhumiwa 10 walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

Pamoja na matukio hayo Lugola amesema anawahakikishia wananchi kwamba nchi yetu ni salama na waendelee na shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila hofu."Jeshi la Polisi linaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kubaini na kuzuia matukio ya uhalifu ukiwemo uhalifu wa utekaji watu.Ni kutokana na juhudi hizo ndio maana wamefanikiwa kuwapata baadhi ya waliotekwa wakiwa hai,"amesema.


Hivyo makala WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA

yaani makala yote WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/watoto-18-wametekwa-nchini-kwa-kipindi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WATOTO 18 WAMETEKWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU-WAZIRI KANGI LUGOLA"

Post a Comment

Loading...