Loading...

WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI

Loading...
WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI
link : WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI

soma pia


WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI

Na. Vero Ignatus, Arusha

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa amelazimika kusitisha ziara kwa masaa mawili na nusu akisubiri kisima katika kijiji cha Levolosi Kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru kinachochimbwa kitoe maji kabla ya kwenda kusaini mkataba.

Aidha Prof. Makame Mbarawa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumrudisha Wizarani mara moja Mhandisi wa Miamba Amir Msangi kwa uzembe wa kutoonekana kwenye eneo la mradi.

Waziri alitoa agizo hilo jana wakati alipotembelea Kijiji cha Levolosi, Kata ya Kimnyaki kujionea zoezi la uchimbaji wa visima vitatu na baada ya hapo alitia saini ya mkataba wa ujenzi wa mtandao mpya wa maji,mitambo ya kutibu maji safi ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA na ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA Kanda ya Kati wenye thamani ya Sh.bilioni 520.

Prof.Mbarawa alisema serikali imeamua kuleta wataalam wake toka Wizarani ili wasimamie na kujifunza Teknolojia mpya ya uchimbaji visima vikubwa kwa ajili ya kuweza kufundiaha wenzao utaalam huo hapo baadaye.

"Lakini cha kushangaza nimepata taarifa huyu Amir Msangi haonekani eneo la kazi na hivyo namwagiza mtaalam mwenzake Fatuma Mambo kumtaarifu Katibu Mkuu ili arudishwe Wizarani huyu na hapa aletwe mwingine atakayepata ujuzi huu,"alisema.Amesisitiza kuwa lengo kubwa la serikali ni kuwaleta wataalam hao ili kuhakikisha miradi ya maji inayotekelezwa inakuwa na ubora uliokusudiwa.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia wananchi kupata maji kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2020.Aidha alisema miradi hiyo inatekelezwa na AUWSA kwa ufadhili wa serikali kupitia mkopo wa masharti nafuu toka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Mhe Mbarawa akiongozwa na wataalamu wa kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd kuangalia mwamba unaotoa maji ardhini kwa kutumia camera maalumu. Picha na Vero Ignatus. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Mbarawa akikagua urefu wa kisima katika kijiji cha Levolosi kata ya Kimnyaki akiwa ameambatana na wahandisi toka wizara ya maji na mamlaka ya maji safi na usafishaji jijinla Arusha AUWSA. Picha na Vero Ignatus


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>


Hivyo makala WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI

yaani makala yote WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/waziri-asitisha-ziara-akisubiri-kisima.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI ASITISHA ZIARA AKISUBIRI KISIMA KITOE MAJI"

Post a Comment

Loading...