Loading...
title : WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU FEDHA ZA DAWA MPWAPWA
link : WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU FEDHA ZA DAWA MPWAPWA
WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU FEDHA ZA DAWA MPWAPWA
*Amuagiza mkuu wa wilaya afanye uchunguzi kubaini zinapokwenda
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Jabir Shekimweri afanye uchunguzi kuhusu matumizi ya sh. milioni 70 zinazotelewa kila mwezi na Serikali kwa ajili ya kununulia dawa kwenye wilaya hiyo.
"Kilichokuwa kinasemwa na wabunge bungeni nilidhani sicho, nikasema nakuja niyasikie mwenyewe. Kweli wananchi hawaridhiki nimeona. Sasa mkuu wa wilaya shughulikia hili jambo ili kubaini fedha za dawa zinakwenda wapi.”
Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Oktoba 10, 2018) wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule msingi Mpwapwa, ambapo alipokea malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa dawa. Dawa pekee wanazopewa ni za kutuliza maumivu tu.
Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali kutoa fedha hizo kila mwezi ni kuhakikisha kwamba wananchi wote wanapata huduma za afya popote walipo badala ya kusafiri umbali mrefu kwenda makao makuu ya wilaya.
"Kila mwezi Serikali inatoa zaidi ya sh milioni 70 kwa ajili ya kununulia dawa kwenye wilaya hii ya Mpwapwa. Pia kuna fedha za mfuko wa afya sh. milioni 60 pamoja na fedha za matokeo mazuri ya afya sh. milioni 300 kwa mwaka, shida ya dawa haitakiwi kuwepo hapa.”
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mpwampwa, kwenye ukumbi wa chuo cha uwalimu Mpwapwa mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwampwa Paul Mamba Sweya, kwenye ukumbi wa chuo cha uwalimu Mpwapwa mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa kwenye uwanja wa Chazugwa mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, akizungumza na wananchi wa Mpwapwa katika uwanja wa Chazugwa mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Marry, akikagua shamba la korosho la Magereza wilayani Mpwapwa Dodoma, Oktoba 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU FEDHA ZA DAWA MPWAPWA
yaani makala yote WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU FEDHA ZA DAWA MPWAPWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU FEDHA ZA DAWA MPWAPWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/waziri-mkuu-abaini-madudu-fedha-za-dawa.html
0 Response to "WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU FEDHA ZA DAWA MPWAPWA"
Post a Comment