Loading...

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awaonya Walimu Kutojihusisha na Wizi wa Mitihani *Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha

Loading...
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awaonya Walimu Kutojihusisha na Wizi wa Mitihani *Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awaonya Walimu Kutojihusisha na Wizi wa Mitihani *Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awaonya Walimu Kutojihusisha na Wizi wa Mitihani *Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha
link : Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awaonya Walimu Kutojihusisha na Wizi wa Mitihani *Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha

soma pia


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awaonya Walimu Kutojihusisha na Wizi wa Mitihani *Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Nyakato wilayani Bukoba baada ya kupokea madarasa ya Shule hiyo yaliyojengwa kwa msaada wa serikali ya Japan. Madarasa hayo yalikabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Mwakilishi wa Balozi wa Japan chini, Bw. Katsutoshi  Takeda 

Madarasa ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikabidhiwa na Mwakilishi wa Balozi wa Japan Nchini, Bw. Katsutoshi Takeda, Oktoba 9, 2018, yaliyojengwa na serikali ya Japan katika Shule ya Misingi ya Nyakato wilayani Bukoba. Madarasa ya shule hiyo yaliharibiwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera.
(Picha n Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya maafisa elimu na walimu kutojihusisha na vitendo vya wizi wa mitihani vinavyofanywa kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kwa sababu vinawadharirisha.

“Kama kweli umemuandaa mtoto huna sababu ya kuiba mitihani na mtoto hawezi kufikiria kuiba mitihani kwa sababu yuko nje ya mfumo. Walimu heshimuni maadili ya kazi ya ualimu.”

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Jumanne, Oktoba 9, 2018) baada ya kukabidhiwa vyumba vya madarasa vya shule za msingi Nyakato na Kashozi, wilayani Bukoba.

Vyumba hivyo vilivyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Japan baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mwaka 2016.

Waziri Mkuu amesema tathmini ya elimu katika shule za msingi na sekondari hufanyika kwa kufanya mitihani, dosari ya udanganyifu wa mitihani iliyojitokeza katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu isijirudie tena.

Wiki iliyopitaBaraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilifuta matokeo ya mitihani ya darasa la saba kwa shule za msingi zote za Halmashauri ya Chemba na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuvujisha mitihani.

Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imechukua hatua kali kwa watu wote walioshiriki katika kitendo hicho kwa sababu kinadumaza uelewa na ufikiri kwa wanafunzi, hivyo kuwaandaa watoto kuwa wategemezi.

“Hata hivyo, Serikali inaendelea na uchunguzi juu ya suala hili ili kubaini chanzo cha wizi huo. Walimu, kitendo cha kumpa mtoto mitihani ni sawa na kujiaibisha kwani mnaonekana hamjafanya kazi zenu ipasavyo. Sitarajii kusikia suala hili tena.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametembelea kiwanda cha kahawa cha Amimza ambacho ni kati ya viwanda vikubwa vitano vya kusindika kahawa Barani Afrika, ambapo ametumia fursa hiyo kumpongeza mwekezaji mzawa Bw. Amiri Hamza na kumuhamasisha aongeze uzalishaji.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametembelea  kituo cha utafiti Maruku ambapo alikagua na kupokea taarifa za shughuli za utafiti wa zao la kahawa na alitumia fursa hiyo kuwashauri wakulima wenye miti mikongwe kung’oa na kupanda mipya kwa awamu.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, OKTOBA  9, 2018.


Hivyo makala Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awaonya Walimu Kutojihusisha na Wizi wa Mitihani *Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha

yaani makala yote Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awaonya Walimu Kutojihusisha na Wizi wa Mitihani *Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awaonya Walimu Kutojihusisha na Wizi wa Mitihani *Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/waziri-mkuu-wa-jamuhuri-ya-muungano-wa_10.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awaonya Walimu Kutojihusisha na Wizi wa Mitihani *Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha"

Post a Comment

Loading...