Loading...
title : Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ameridhishwa na Hatua za Awali Uwekezaji Mkinga
link : Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ameridhishwa na Hatua za Awali Uwekezaji Mkinga
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ameridhishwa na Hatua za Awali Uwekezaji Mkinga
Na.Khadija Mussa .OWM.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea eneo la mradi wa ujenzi wa viwanda 11 katika kijiji cha Mtimbwani wilayani Mkinga, ambapo amesema ameridhishwa na hatua za awali za uwekezaji huo.
Katika eneo hilo vinatarajiwa kujengwa viwanda mbalimbali kikiwemo cha saruji cha Hengya, kiwanda cha vioo, kiwanda cha vifaa vya kisasa vya ujenzi, uzalishaji wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Oktoba 30, 2018) wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mtimbwani wilayani Mkinga akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga.
Amesema uwekezaji huo unatarajiwa kulinufaisha Taifa na wananchi wakazi wa wilaya ya Mkinga kwa kuwa kinatarajiwa kuajiri zaidi ya watu 8,000, hivyo amewaomba wananchi hao waendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hao.
Kuhusu wananchi ambao eneo lao limechukuliwa na wawekezaji na bado hawajalipwa fidia Waziri Mkuu amewataka wawe na subira kwa kuwa wote watalipwa. “Muwekezaji amenihakikishia kwamba atawalipa wananchi wote wanaodai fidia.”
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuuamewataka watumishi wa umma kutenga siku tatu katika wiki na kuwafuata wananchi waishio maeneo ya vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.
Amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi wa kidini, kisiasa, rangi na kimapato, hivyo amewataka watumishi hao wafanye kazi kwa bidii.
Awali, Mbunge wa jimbo la Mkinga, Dastan Kitandula ameishukuru Serikali kwa niaba ya wananchi wa Mkinga baada ya Serikali kufuta hati ya shamba la moa na kuirudisha ardhi hiyo kwa wananchi, pia ameomba ifute hayi za mashamba mengine yaliyotekelezwa katika Tarafa ya Maramba.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, OKTOBA 30, 2018.
Hivyo makala Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ameridhishwa na Hatua za Awali Uwekezaji Mkinga
yaani makala yote Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ameridhishwa na Hatua za Awali Uwekezaji Mkinga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ameridhishwa na Hatua za Awali Uwekezaji Mkinga mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/waziri-mkuu-wa-jamuhuri-ya-muungano-wa_17.html
0 Response to "Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ameridhishwa na Hatua za Awali Uwekezaji Mkinga"
Post a Comment