Loading...

Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon

Loading...
Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon
link : Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon

soma pia


Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon

Mwanza, 9 Oktoba 2018: Washindi wa michuano ya Rock City Marathon 2018 wanatarajiwa kuondoka na zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 30 pamoja na medali, imefahamika. Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizungumza jijini Mwanza leo, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo zinazoratibiwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Zenno Ngowi alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na medali na pesa taslimu.

Kwa upande wa mbio za Kilomita 21, Ngowi alisema, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 3/- kila mmoja, sh. Mil 1/- kwa washindi wa pili na sh. 750,000/- kwa washindi wa tatu huku washindi wanne hadi wa kumi wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.

“Mbio za kilomita tano tunatarajia kwamba zitaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza sambamba na baadhi ya wakuu wa mikoa kanda ya Ziwa ambao pia watajumuika na baadhi ya viongozi waandamizi wa mikoa hiyo wakiwemo wabunge, viongozi na wafanyakazi wa mashirika na makampuni mbalimbali yaani corporates pamoja na ndugu zetu wenye ualbino,’’alisema.

Wadhamini watakaoshiriki katika mbio hizo ni pamoja na kampuni za Puma Energy Tanzania, Tiper, TANAPA, TTB, Nssf, Gold Crest, New Mwanza Hotel, Cf Hospital, CocaCola, Metro Fm, Ef Outdoor, Kk Security, Belmont Fairmount Hotel , Bigie Customs na Global Education Link.

Alibainisha kuwa mbio za Km 5 zitahusisha watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino ambapo washindi kwa upande wa mashirika watapatiwa zawadi za utambuzi ikiwemo medali na vyeti vya ushiriki huku pesa zikielekezwa kwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.
Baadhi ya Washiriki waliowahi kushiriki mashindano hayo ya Rock City Marathon.



Hivyo makala Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon

yaani makala yote Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/zawadi-za-milioni-30-kushindaniwa-rock.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Zawadi za milioni 30 kushindaniwa Rock City Marathon"

Post a Comment

Loading...