Loading...
title : ASILIMIA 30 SAWA NA KAYA MASKINI 6,048 HAZIJAFIKIWA -TASAF
link : ASILIMIA 30 SAWA NA KAYA MASKINI 6,048 HAZIJAFIKIWA -TASAF
ASILIMIA 30 SAWA NA KAYA MASKINI 6,048 HAZIJAFIKIWA -TASAF
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA .
MKURUGENZI wa mfuko wa maendeleo ya jamii -TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema, bado zipo kaya maskini 6,048 sawa na asilimia 30 Tanzania Bara na Visiwani, ambazo hazijafikiwa katika utekelezaji wa mpango kunusuru kaya maskini .
Aidha , wale ambao wameshanufaika awamu ya kwanza ya mpango huo watafanyiwa tathmini, na wameandaa mkakati wa kuwapima kwa vigezo vya kuwa na hali nafuu kwa utaratibu ili watoke na wapishe wengine.
Akiweka bayana juu ya masuala hayo, wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani, alisema maeneo ambayo hayakufikiwa ,utekelezaji utaanza mwezi april 2019 ,ili kukamilisha maeneo yote nchi nzima 16,048.#
Mwamanga alisema vijiji,sheia na mitaa 10,000 wameshavifikia hadi sasa .
Alifafanua, kuna kaya maskini ziliachwa kwenye mpango kwa sababu mbalimbali nao wataingizwa kwenye mfumo thabiti ili kuwa na rekodi sahihi kwa nchi nzima. Hata hivyo ,alisema kaya ambazo zina wazee na wenye ulemavu wataendelea kuwasaidia ili kukidhi mahitaji yao ya msingi.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N’hunga alisema, serikali ipo katika hatua za mwisho za kisera kutatua changamoto ya muda mrefu kwa kaya ambazo hazikujumuishwa katika mpango .
Kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii Ladislaus Mwamanga (mwenye suti ya rangi ya ugolo) na baadhi ya viongozi mkoani Pwani na halmashauri ya Kibaha Vijijini, wakipatiwa maelezo wakati walipotembelea kilimo cha bustani huko Disunyara Kibaha Vijijini. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Naibu waziri ,ofisi ya makamu wa pili Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mihayo N’hunga akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia ofisi ya viongozi wakuu wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika Kibaha Vijijini Mkoani Pwani. (picha na Mwamvua Mwinyi) .
Hivyo makala ASILIMIA 30 SAWA NA KAYA MASKINI 6,048 HAZIJAFIKIWA -TASAF
yaani makala yote ASILIMIA 30 SAWA NA KAYA MASKINI 6,048 HAZIJAFIKIWA -TASAF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASILIMIA 30 SAWA NA KAYA MASKINI 6,048 HAZIJAFIKIWA -TASAF mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/asilimia-30-sawa-na-kaya-maskini-6048_15.html
0 Response to "ASILIMIA 30 SAWA NA KAYA MASKINI 6,048 HAZIJAFIKIWA -TASAF"
Post a Comment