Loading...
title : BARAZA LA TIBA ASILI LATOA ELIMU KWA WAKUNGA WA JADI
link : BARAZA LA TIBA ASILI LATOA ELIMU KWA WAKUNGA WA JADI
BARAZA LA TIBA ASILI LATOA ELIMU KWA WAKUNGA WA JADI
NA WAMJW- DAR ES SALAAM.
BARAZA Tiba asili na Tiba mbadala nchini limetoa elimu kwa wakunga wa jadi kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha mama mjamzito anajifungua salama kwenye kituo cha afya kilichopo karibu ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Hayo yamesemwa na Msajili wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala nchini Dkt. Ruth Suza wakati wa semina na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa tiba asili na tiba mbadala nchini.
Amesema kuwa wakunga wa jadi nchini wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuhakikisha wamama wajawazito wanawahimiza kujifungulia katika vituo vya afya kwa usalama wa maisha ya mama na mtoto.
"Tunapita kuwaelimisha Wakunga wa jadi kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha mama mjamzito anajifungua salama kwenye kituo cha afya kilichopo karibu ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi" alisema Dkt. Suza. Dkt Suza amesema jumla ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala 19912 wamesajiliwa na Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala nchini ili kuweza kutoa huduma hizo kwa kufuata sheria na taratibu.
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk.Edmond Kayombo akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu taratibu na hatua za usajili wa waganga,dawa na vituo vyakutolea huduma leo jijini Dar es Salaam, (kushoto ni)Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Mratibu wa Taifa tiba asili na tiba Mbadala Dkt.Liggyle Vumilia wa Wizara ya Afya akizungumza na waandishi habari na wadau mbalimbali juu hatua walizozichukua kwa watoaji huduma tiba asili na tiba mbadala leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Mfamasia Baraza la tiba asali na tiba Mbadala wa Wizara ya Afya, Ndahani Msigwa akizungumza na wadau mbalimbali wa afya kuhusu sheria, kanuni na taratibu za utoaji huduma za tiba mbadala leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu wa wadau mbalimbali wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk. Edmond Kayombo.
Picha ya pamoja
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala BARAZA LA TIBA ASILI LATOA ELIMU KWA WAKUNGA WA JADI
yaani makala yote BARAZA LA TIBA ASILI LATOA ELIMU KWA WAKUNGA WA JADI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BARAZA LA TIBA ASILI LATOA ELIMU KWA WAKUNGA WA JADI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/baraza-la-tiba-asili-latoa-elimu-kwa.html
0 Response to "BARAZA LA TIBA ASILI LATOA ELIMU KWA WAKUNGA WA JADI"
Post a Comment