Loading...
title : BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WAKE SHINYANGA
link : BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WAKE SHINYANGA
BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WAKE SHINYANGA
Benki ya NMB imeendesha mafunzo kwa Mawakala NMB mkoa wa Shinyanga kwa ajili kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafahamu mbinu za kudhibiti fedha haramu pamoja na mbinu za kukuza biashara zao kwa kuongeza wateja.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni alikuwa Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Melusori alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwawezesha mawakala kukuza kipato chao lakini pia namna ya kudhibiti fedha chafu/haramu ‘Money laundering’.
“Lengo jingine ni kuwasilisha na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili mawakala hawa,kuwapongeza/kutambua mchango wa mawakala wanaofanya kazi vizuri na kuwaeleza kuhusu maboresho yanayofanywa na NMB”,alisema Melusori.
Hata hivyo aliwataka mawakala wa NMB kufanya kazi kwa umakini na kuzingatia maadili katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria halali za fedha.“Asilimia ya watanzania wanaotumia benki ipo chini ya asilimia 20 kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni hivyo shirikiane na benki kuhakikisha kuwa watanzania ambao hawajaanza kutumia huduma ya benki kwani benki ni sehemu salama zaidi”,aliongeza.
Hivyo makala BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WAKE SHINYANGA
yaani makala yote BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WAKE SHINYANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WAKE SHINYANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/benki-ya-nmb-yatoa-mafunzo-kwa-mawakala.html
0 Response to "BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WAKE SHINYANGA"
Post a Comment