Loading...

DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA

Loading...
DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA
link : DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA

soma pia


DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA

Na Is-Haka Omar, Zanzibar
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema endapo Wabunge na Wawakilishi watashindwa kutumia fedha za maendeleo ya mfuko wa jimbo zinazoingizwa katika Halmashauri za Wilaya, CCM itachukua hatua ya kuidhinisha fedha hizo zitumike kutatua kero sugu zinawakabili wananchi.

Msimamo huo ameutoa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 katika Halmashauri ya Wilaya Kusini Unguja, amesema fedha za mfumo wa maendeleo ya Jimbo ni haki ya wananchi na sio fedha za viongozi wa jimbo. Amesema viongozi hao  wanakabidhiwa fedha hizo kwa ajili ya kusimamia utaratibu wa matumizi yake na sio kuziacha katika akounti za benki bila kutumika hali inayosababisha kutokamilika kwa baadhi ya miradi ya wananchi.

Dk. Mabodi akikagua miundombinu ya vyoo katika skuli ya Sekondari na Msingi ya Kusini Makunduchi alikuta skuli hiyo ina changamoto ya upungufu wa vyoo huku wanafunzi na walimu wakitumia vyoo chakavu, na kuamua kutoa agizo kwa Halmashauri kuidhinisha kiasi cha shilingi milioni 10 kutoka fedha za maendeleo ya jimbo hilo zilizokaa muda mrefu bila ya kutumiwa. Pia Naibu Katibu Mkuu kupitia Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein aliahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya matengenezo ya haraka ya miundombinu ya vyoo hivyo kuhu akisisitiza viongozi wa Chama na Serikali kuchukua hatua za makusudi kumaliza changamoto za aina hiyo katika skuli mbali mbali za Unguja na Pemba.

Akiwa katika skuli hiyo alitoa wito kwa viongozi wa Chama na Serikali kushuka kwa wananchi hasa wa vijijini kuangalia changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu kwa mujibu wa maelekezo yaliyomo katika Ilani ya CCM. Aidha Dk.Mabodi akiwa katika shamba la kuotesha miti mbali mbali ikiwemo ya Matunda huko katika Kijiji cha Mungoni, alishauri wananchi wanaofanya shughuli hizo kuhakikisha wanaotesha miti inayotoa matunda yenye soko  ikiwemo miti aina ya midimu.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi wakati akikagua ukarabati wa Kituo cha Afya Mungoni aliitaka Halmashauri kuharakisha ujenzi huo ili wananchi waendelee kupata huduma bora za Afya. Pamoja na hayo Naibu Katibu Mkuu aliipongeza Halmashauri ya Kusini Unguja kwa kutekeleza vizuri miradi ya ujenzi wa vyoo na madarasa ya kisasa katika Skuli za Mtende na Bwejuu yaliyotekelezwa kupitia mpango wa ugatuzi wa madaraka kupitia Serikali za Mitaa.
 MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja Kassim Mtoro Abu (wa kwanza kushoto) akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Ilani katika Halmashauri hiyo kwa mwaka 2015/2018, Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib Hassan (wa pili kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi (wa kwanza kulia).
  NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Dk. Abdulla Juma Mabodi akiwa katika ziara ya katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja uliotekelezwa chini ya mpango wa ugatuzi.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Dk. Abdulla Juma Mabodi akikagua maendeleo ya Kikundi cha wanawake cha ujasiriamali cha Furahia kilichopo Kijiji cha Paje ambacho kinanufaika na miradi ya uwezeshaji iliyopo katika mpango wa ugatuzi.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Dk. Abdulla Juma Mabodi akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja pamoja na Viongozi wa CCM wa Jimbo, Wilaya na Mkoa wa Kusini Unguja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA

yaani makala yote DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/dkt-mabodi-afanya-ziara-wilaya-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT. MABODI AFANYA ZIARA WILAYA YA KUSINI UNGUJA"

Post a Comment

Loading...