Loading...
title : DKT. NDUGULILE AIPONGEZA TAASISI YA NIMR KWA TAFITI ZENYE TIJA KWA TAIFA
link : DKT. NDUGULILE AIPONGEZA TAASISI YA NIMR KWA TAFITI ZENYE TIJA KWA TAIFA
DKT. NDUGULILE AIPONGEZA TAASISI YA NIMR KWA TAFITI ZENYE TIJA KWA TAIFA
Na WAMJW- Muheza, Tanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) kwa kufanya tafiti nzuri zinazoisaidia serikali katika mabadiliko ya sera ya afya kwenye matibabu ya ugonjwa wa Malaria
Dkt. Ndugulile amtoa pongezi mara baada ya kutembelea katika kituo cha tafiti cha ya ugonjwa wa Malaria Nirmi kilichopo katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga. “Serikali tunajivunia kuwa na taasisi hii, katika udhibiti wa ugonjwa wa Malaria tumepiga hatua kubwa, tumepunguza maambukizi ya Malaria kwa zaidi ya asilimia 50, tulikuwa na asilimia 14 sasa hivi tuna asilimia 7. Kwa juhudi ambazo tunaenda nazo katika tafiti hizi naamini kiwango cha maambukizi kitaendelea kushuka.” Alisema Dkt Ndugulile.
Licha ya kunufaika na tafiti hizo, Serikali imejiwekea malengo ya kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria nchini, Dkt Ndugulile amesema kuwa Serikali imejiwekea mikakati mbalimbali ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria kwa kutoa vyandarua, dawa za kuuwa vimelea vya Malaria, kila mgonjwa kupimwa ugonjwa wa Malaria pamoja na kunyunyizia dawa katika makazi ili kuuwa mazalia ya mbu. Aidha Dkt. Ndugulile ameipongeza taasisi hiyo ya Nimr kwa kutambulika na mashirika ya kimataifa kutokana na tafiti inazozifanya kuwa na ubora wa hali ya juu. “Niwapongeze kwa tafiti zetu kutambulika kimataifa, siyo tuu kwa kutusaidia katika mabadiliko ya sera bali pia
“Tafiti zetu zinatambulika kimataifa, hivi sasa kituo hiki kinatambulika na Shirika la Afya Duniani (WHO) kutokana na tafiti mbalimbali kuhusiana na ugonjwa wa Malaria, kwa hiyo nawapongeza wote kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya” alisema Dkt Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia sampuli za mbu katika maabara ya Taasisi ya Nimr Muheza, Tanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo (kushoto) alipotembelea kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu Nirmr.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia vifaa vya zamani vilivyotumika kufanya tafiti katika kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu Nirmr Amani Muheza.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia lililokuwa jengo la posta ya zamani kabla ya uhuru ambalo lipo katika ofisi za Nimri Amani, Muheza.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisoma kitabu cha tafiti za zamani katika kituo cha tafiti Nimr Amani, Muheza.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala DKT. NDUGULILE AIPONGEZA TAASISI YA NIMR KWA TAFITI ZENYE TIJA KWA TAIFA
yaani makala yote DKT. NDUGULILE AIPONGEZA TAASISI YA NIMR KWA TAFITI ZENYE TIJA KWA TAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT. NDUGULILE AIPONGEZA TAASISI YA NIMR KWA TAFITI ZENYE TIJA KWA TAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/dkt-ndugulile-aipongeza-taasisi-ya-nimr.html
0 Response to "DKT. NDUGULILE AIPONGEZA TAASISI YA NIMR KWA TAFITI ZENYE TIJA KWA TAIFA"
Post a Comment