Loading...
title : HAKUNA MGAO WA UMEME MWAKA HUU -DKT ALEXANDER KYARUZI
link : HAKUNA MGAO WA UMEME MWAKA HUU -DKT ALEXANDER KYARUZI
HAKUNA MGAO WA UMEME MWAKA HUU -DKT ALEXANDER KYARUZI
Na Francis Godwin,Iringa
MWENYEKITI wa bodi ya shirika la umeme Tanzania (TANESCO ) Dkt Alexander Kyaruzi amesema kuwa hali ya uzalishaji wa umeme nchini ni nzuri na kuwa watanzania wasitegemee kuwepo kwa mgao wa umeme kwa mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla ya uwashaji umeme kijiji cha Ndolezi katika Halmashauri ya mji Mafinga Dkt Kyaruzi alisema kuwa pamoja na kuwa kipindi cha kiangazi kinakwenda kumalizika ila hali ya maji katika vituo vya uzalishaji umeme vya Kidatu na Mtera ni nzuri na kuwa maji hayo yataendelea kuongezeka zaidi kwani msimu wa masika unakaribia.
Kuhusu kasi ya usogezaji wa umeme katika vijiji ,vitongoji na maeneo ya visiwa alisema kuwa kasi inaendelea vizuri na kuwa hadi mwaka 2021 maeneo yote ya nchi umeme utakuwa umefika na hakutakuwa na kijiji wala kisiwa ambacho wananchi watakuwa hawana umeme .
Pamoja na umeme huo wa maji na gesi ambao unatumika kwa sasa bado alisema shirika limeendelea na uvumbuzi wa vyanzo vingine vya umeme kama umeme wa joto ardhi ambao tafiti zinaonyesha baadhi ya mikoa kama mkoa wa Mbeya kuwepo kwa umeme huo .
" Tunategemea miaka mitano mbele kuwa na umeme utakaozalishwa kupitia joto ardhi hivyo bado nchi itaendelea kuwa na uhakika wa umeme baada ya kuwa na vyanvyo tofauti tofauti " alisema Dkt Kyaruzi
Alisema kuwa maeneo Ziwa ngozi mkoani Mbeya ni eneo la kwanza ambalo wamefanikiwa kufanya utafiti na kuonekana lina weza kuzalisha umeme wa joto ardhi na tayari wamempata mkandarasi wa kufanya zoezi la uchimbaji wa eneo hilo .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ali Hapi mwenye suti nyeusi na mkurugenzi wa bodi ya Tanesco Dkt Alexander Kyarusi kulia wakiwasha umeme kijiji cha Ndolezi Mafinga mkoani Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi akisikiliza kero za wananchi juu ya umeme wilayani Mufindi jana
Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco Dkt Alexander Kyaruzi (kushoto) akifuatilia taarifa ya meneja wa Tanesco Mafinga wakati wa uwashaji umeme kijiji cha Ndolezi
Wananchi Mufindi wakitoa kero zao kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi wakati wa kuwasha umeme kijiji cha Ndolezi Mafinga.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
Hivyo makala HAKUNA MGAO WA UMEME MWAKA HUU -DKT ALEXANDER KYARUZI
yaani makala yote HAKUNA MGAO WA UMEME MWAKA HUU -DKT ALEXANDER KYARUZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HAKUNA MGAO WA UMEME MWAKA HUU -DKT ALEXANDER KYARUZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/hakuna-mgao-wa-umeme-mwaka-huu-dkt.html
0 Response to "HAKUNA MGAO WA UMEME MWAKA HUU -DKT ALEXANDER KYARUZI"
Post a Comment